GET /api/v0.1/hansard/entries/258190/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 258190,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/258190/?format=api",
    "text_counter": 465,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "The Minister for Youth Affairs and Sports",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Siasa za kuvutana hazina nafasi katika Kenya ya sasa. Hakuna haja ya sisi kubishana na kusema sisi ni bingwa kuliko wale na kadhalika. Tunahitaji siasa za kujenga na kuleta maendeleo katika nchi hii. Hakuna aliyeshabiki au bingwa kuliko mwingine katika Serikali hii. Wakenya wametupa nafasi hii ili tuweze kuwatumikia tukiwa pamoja. Tunashirikiana pamoja hapa Bungeni na Serikalini ili tuweze kutatua matatizo mengi yanayowakumba wananchi wetu. Kuna baadhi ya viongozi wanaopenda kushabikia maswala ambayo hawayaelewi vilivyo. Sisi kama waheshimiwa Wabunge tunahitajika kufanya kazi pamoja ili wananchi wetu wapate afueni ya shida zinazowakumba maishani. Wakati umefika kwa sisi kwenda kuungana na wananchi kule mashinani ili tusheherekee pamoja siku kuu hii ya Krimasi na kuukaribisha mwaka mpya. Maswala ambayo yamezungumziwa na Naibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha, Bw. Uhuru Kenyatta, ni mazito na yanahitaji sisi sote kuyashughulikia kwa wakati ufaao. Haifai sisi kuyashughulikia kwa haraka na kwa muda mfupi. Maswala haya yanahitaji wakati wa kutosha. Kwa hivyo, tunataka kwenda likizo ili tuweze kuungana na ndugu zetu Wakristo wakati huu wa Krismasi na baada ya mwaka mpya na kuhakikisha kwamba Wakenya wamefaidika."
}