GET /api/v0.1/hansard/entries/261664/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 261664,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/261664/?format=api",
    "text_counter": 53,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wanahusika na Mazingira wataweza kutoa kandarasi. Hata hivyo, katika sehemu hii ya Mheshimiwa Eng. Rege, tayari tumetumia Kshs26 milioni kwa Kshs170 milioni ambazo tumeweza kupewa kama ruzuku na Umoja wa Mataifa na Benki Kuu ya Ulimwengu. Jambo ambalo ningependa niseme kinaga ubaga ni kwamba Wizara zote Afrika Mashariki za mazingira ni kwamba zitafanya huu mradi bila tashwishi yoyote. Bw. Spika, unaweza kukumbuka kwamba Swali hili nimelijibu mara nyingi katika Bunge hili lakini pia sioni vibaya mara kwa mara kwa sababu kuna maeneo matano ya ubunge ambayo yana shida ya magugu ama kwa kimombo “hyacinth”. Kwa hakika, sisi tunaendelea kufanya kazi hiyo. Baraza la Mawaziri Afrika Mashariki limeonyesha kuhusika kwake na ningependa kusema kwamba mradi huu utatengenezwa kama vile Eng. Rege anavyotumaini."
}