GET /api/v0.1/hansard/entries/261707/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 261707,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/261707/?format=api",
    "text_counter": 96,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kajembe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 163,
        "legal_name": "Ramadhan Seif Kajembe",
        "slug": "ramadhan-kajembe"
    },
    "content": "Bw. Spika, Ziwa Victoria zinasimamiwa na nchi tano nazo ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi. Swala la kurekebisha Ziwa Victoria hupitiwa tu katika Baraza la Mawaziri wa Mazingira wa Afrika Mashariki. Swala hili limezungumzwa vya kutosha na kuna mkataba ambao umefikiwa kati ya nchi hizi tano za Afrika Mashariki, kwamba Benki kuu ya Ulimwengu itatoa pesa katika mafungu manne ili kuondoa hii kwekwe katika Ziwa Victoria. Pia, serikali zinazohusika za Afrika Mashariki zilipewa nafasi yao, kwamba zitaongeza pesa kusafisha hii Kwekwe. Mpaka sasa, Benki Kuu ya Ulimwengu imetoa Kshs178 milioni wakati tunangoja pesa nyingine za Serikali kuu. Hata hivyo, wakati umefika tuingie katika sehemu ya pili na Benki Kuu ya Ulimwengu ili tuleta pesa tuendelee kusafisha hii kwekwe katika Ziwa Victoria. Ninataka niseme kuwa katika mikutano ya Mawaziri wa nchi tano za Afrika Mashariki ambayo mimi pia ninahudhuria, kila kitu kinaendelea sawasawa."
}