GET /api/v0.1/hansard/entries/262249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 262249,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/262249/?format=api",
    "text_counter": 118,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Mswada huu. Ninaomba nitoe pongezi zangu kwa mhe. Waziri wa Serikali za Wilaya na Mitaa kwa kazi yake nzuri ya kuwasilisha Mswada huu mbele ya Bunge hili. Ninaunga mkono Mswada kwa vile umezingatia maadili na uzito wa Katiba yetu. Mswada huu umetilia mkazo swala la ugatuzi. Tumekuwa tukipigania ugatuzi tangu mwaka wa 1963 nchi yetu ulipopata Uhuru. Tunaweza kukumbuka vizuri kuwa miaka michache baada ya Uhuru, Serikali ya Majimbo haikuweza kufanya kazi vilivyo kwa sababu ilipigwa vita na Serikali kuu. Hii ni kwa sababu viongozi wa Serikali kuu hawakutaka Serikali ya Majimbo. Ilibainika wazi kuwa matakwa ya Serikali kuu au viongozi wake hayakwenda sambaba na matakwa ya wananchi. Serikali za majimbo zilinyimwa pesa za kuendesha shughuli zao. Kwa hivyo Serikali hizo hazikufanya kazi za kuwahudumia watu wake. Wakati huu, ugatuzi wetu unajulikana kama County Governments. Hizi ni Serikali za Wilaya na Mitaa ambazo zimeunganishwa pamoja kuunda kaunti moja. Kwa mfano, tuna kaunti ya Taita Taveta. Kaunti hii imebuniwa baada ya kuunganisha Wilaya ya Taita na Wilaya ya Taveta. Mimi kama mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Serikali za Wilaya nimekubana na shida nyingi sana kutoka kwa miji na mitaa mingi hapa nchini. Tunapojadili akaunti zao, tumekuta mambo mengi ya kustaajabisha. Kwa hivyo, ni ombi langu kuwa Waziri wa Serikali za Wilaya na Mitaa asikilize kwa makini yale yote nitakayoyasema. Hii ni kwa sababu tumekubana na mambo mengi sana. Jambo la kwanza ni kuwa Serikali hizi hazihifadhi vitabu ya matumizi ya pesa zao. Hakuna stakabadhi za kuonyesha kuwa hesabu zao zimekaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Vitabu vya Serikali. Serikali hizi hazijahifadhi stakabadhi kwa makini. Kila kitu kimeweka holelahola. Kwa hiyo, gavana ambaye atachaguliwa atarithi Serikali za Wilaya ambao hazijawahi kuweka stakabadhi ya matumizi ya pesa kwa miaka mingi. Mambo ya fedha katika serikali hizi hayajawahi kutiliwa mkazo. Kama tunavyojua rasilmali za wilaya ni nyingi. Hata hivyo hakuna mtu ambaye ana hesabu ya rasimali hizo katika wilaya nyingi. Tulitarajia kuwa Serikali za Wilaya zitakuwa zimeweka stakabadhi, vitabu na rejesta zao vizuri ilikuonyesha wapi, rasilmali hizi ziko. Tungependa kuona ploti za wilaya hii ziko wapi. Ni nani ana stakabadhi hizo ploti na kadhalika. Jambo la kuhuzunisha ni kuwa hakuna aliye na stakabadhi hizo. Sababu ni nini? Hawawezi kuzihifadhi kwa sababu nia yao kubwa ni ulaghai ili wazipore na waweze kuziuza. Serikali za Ugatuzi zitajishughulisha na swala la rasilmali za wilaya. Lakini swali nyeti ni kuwa waanzia wapi na kumalizia wapi kwa vile hakuna stakabadhi za kutosha. Katika kazi yetu ya Kamati tumekubana na wizi wa kustaabisha katika Serikali za Wilaya. Unakuta pesa za LATF au zilizotengewa kujenga barabara zimeibiwa. Hakuna rekodi za kuonyesha jinsi pesa hizo zilitumika. Madiwani wanafanya kazi kiholela. Maofisa wakuu ambao wamepelekwa huko pia nao wanafanya kazi kiholela. Kwa hivyo, wasiwasi wangu mkubwa katika ugatuzi huu ni kuwa tunaunganisha Serikali za Wilaya kuwa kaunti moja lakini hakuna stakabadhi. Ninamuomba Waziri ahakikishe kuwa Serikali zote za wilaya zimeweka stakabadhi zao vizuri. Ni lazima ahakikishe mabaraza yote yameweka stakabadhi ili gavana na baraza lake wataweza kuendesha shughuli zao vilivyo. Ujenzi wa barabara unaendelea katika kaunti. Kuna mashirika ambayo yanahusika na ujenzi wa barabara hizo lakini hakuna stakabadhi ya kuonyesha hawa ni akina nani. Je, mashirika haya yatandelea na ujenzi wa barabara hizo? Hilo ndilo swali kubwa kwetu. Na kama yatakuwepo mamlaka yake yatakuwa tukilinganisha na mamlaka ya Gavana. Katika kuzunguka kwetu na katika kupokea maoni kutoka kwa haya mabaraza, tumekuta uajiri ni kitu kingine ambacho kimeleta kero sana. Wale watu ambao wanaajiriwa katika mabaraza ya wilaya imekuwa watu wanaajiri ndugu zao. Ninashukuru katika Mswada huu, umeweka wazi wazi kua wale watakao ajiriwa watakuwa watu ambao wanasifa za kutosha, wamehitimu na wanaweza hizi kazi. Ingikuwa sio hivyo tungekuta hivyo hivyo haya mambo ambayo tumeyakuta katika mabaraza ya wilaya ndio haya haya yanapelekwa katika serikali za kaunti. Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaomba hata uajiri, wale ambao watakuwa wamepewa nafasi za kuajiri wenzao wahakikishe kuwa hao watakaoajiriwa katika serikali za kaunti wawe ni watu ambao wanasifa, wanidhamu na ni watu ambao wanaweza kutekeleza wajibu wao kama inavyo pasa. Mapato katika serikali hii mpya, tumeangalia na kuona kwamba serikali za kaunti zitakuwa na uwezo wa kutoza ushuru fulani. Ushuru huu ni muhimu uangaziwe kwa sababu usipoangaziwa vizuri kihundi ya fedha ambao utakuwa unatoka katikaSerikali Kuu utakuwa peke yake haitoshi kuendeleza kazi za serikali ya kaunti. Kwa hivyo, ushuru kama ushuru wa madini, mazao ya shamba, barabara na kadhalika ni lazima utozwe na uingie ndani ya serikali ya kaunti. Isipofanywa hivyo, kama ni huu ulaghai ambao tumeikuta katika mabaraza ya wilaya, tutakuwa tumetoa ugonjwa katika mabaraza ya wilaya na tukaupeleka katika serikali ya kaunti na tutakuwa hatufanyi chochote. Bw. Naibu Spika wa Muda, huyu ndugu ambaye tunamuita Gavana tukiangalia Katiba imetupatia serikali mbili; Serikali ya Ugatuzi na Serikali Kuu. Kwa nini Gavana atapokea maagizo kutoka kwa Rais? Kama ni Gavana basiawena mamlaka yake, ashugulikie kaunti yake, amechaguliwa na wananchi na ashugulike kikamilifu vile inavyowezekana. Kwa hivyo ni muhimu mamlaka makuu yapewe Gavana . Awenaweza kufanya kazi zake bila kutatizwa ama uanza kusema, “Nimeambiwa na Rais nifanye hili jambo”. Ile karne tulikuwa nayo kuwa, “Nimepewa amri kutoka juu” hatuitaki tena. Tunataka Gavana awe ni Gavana anaweza kushughulia kazi zake, amechaguliwa na wananchi na atumikie wananchi. Nimesikia wenzangu wakizungumuzia kwa lugha ya kimombo kuhusu kama kutakuweko na bendera. Sawa, ni serikali. Kama Serikali Kuu ina bendera yake kwa nini serikali ya ugatuzi uko chini isiwe na bendera yake? Kuna shida gani? Labda swala ambalo litakalo tokea pia, wakiwa na bendera yao, watakuwa na wimbo wao wa kaunti? Nini kitakacho wazuia wasiimbe wimbo wao wa kaunti? Katika Katiba haijazuiliwa! Kwa hivyo, kama watakuwa na bendera yao ya kaunti na wimbo wao wa kaunti uwekwe. Nyimbo zote mbili zinaweza kuimbwa; mkaimba wimbo wa taifa na muimbe wimbo wa kaunti yenu kwa sababu ni kautni yenu. mnaipatia sifa, mnaiinua. Kwa nini muone haya kuwa na wimbo wenu wa kaunti? Kwa Kizungu tunasema identity. Tukisimama katika Kaunti ya Taita Taveta tunataka tuimbe wimbo wetu wa Kaunti ya Taita Taveta kwa sababu tunajivunia ile asili yetu. Na wenzetu wakiwa na bendera yao, kama ndugu yangu amesema juu ya Kericho; bendera yao anataka iwe na rangi ya majani kwa sababu wanajani, sawa nao pia wawe na bendera yao ya majani. Hatuna shida. Sisi Taita tutakuwa na bendera yetu. Tunamadini na kila kitu. Kwa hivyo ninaomba, Waziri, ukiwa unaangalia Mswada huu, uangalie kuwa Gavana amepewa mamlaka. Bw. Naibu Spika wa Muda, hadi sasa hatujajua kikamilifu kwa kuwa fedha zitatolewa za kutosha za kujenga makao makuu. Tumezunguka tukakubaliana kwamba kila kaunti itakuwa na makao makuu lakini sio kaunti zote ambazo zinamakao makuu ambazo yako tayari. Bila shaka zitatumia zile rasilimali; nyumba, nafasi na maofisi ambayo yalikuwa yanatumia hapo awali huku wanajitayarisha kujenga makao yao makuu. Lakini hata tukisema hivyo litakuwa ni jambo la kufadhaisha kama kila kaunti itatarajiwa itowe zile fedha imepewa za kujiistiri ziwe ni za kujenga makao makuu. Itakuwa hizo fedha hazitawasaidia. Kwa haya mengi, ninaunga mkono Mswada huu. Ufanyiwe marekebisho hasa kuhusu rasili mali. Ifanyiwe marekebisho kuhusu vipengele ambavyo wale watakuwa wamevunja sheria za uwekezaji waadhibiwe. Wale watu ambao wako na rasilimali, tukizunguka nchi yote utakuta watu wako na rasili mali za aina tofauti tofauti. Kama sisi Taita tukona madini. Jee ni fedha kiasi gani tutazipata kwa madini yetu ambazo zitaingia kwa kaunti? Sikatai kwamba Katiba inasema kuwa madini yote ni ya Serikali lakini lazima kuwe na ugawaji. Yale mambo tumeyaona miaka ambao imepita hadi sasa has nikiangalia sheria ya kuvuna madini. Hivi sasa mtu mwenye mgodi anaweza kuvuna na hatakiwe na Serikali wala hakuna sheria yeyote ya kumushurutisha agawanyie Serikali chochote. Atavuna, aweke kwa lori aende nayo. Tunasema tuangalia, katika rasilimali ambazo ziko katika kaunti, wenyeji wa kaunti wanafaidika katika hizo rasilimali, Serikali inafaidika na Kaunti yenyewe inafaidika. Tusije tukawa na tatizo kwamba unakuta kaunti inamali lakini mali yote inaenda kwa Serikali kuu. Hatutaki kuona mambo kama ambayo tunayaona Pwani hivi sasa. Rasilimali tulizonazo ni nyingi, utakuka kitu kama bandari iko Mombasa lakini angalia hali ya ndungu zetu wa Likoni. Hauwezi kuamini kwamba bandari iko kwao. Tunaomba tukiingia katika ugatuzi wale watu wamejaliwa kuwa na rasilimali--- Na ni nyingi hakuna kaunti imenyimwa rasilimali na Mungu, lakini kama rasilimali zote zitaenda katika Serikali Kuu basi huu ugatuzi hautakuwa na maana. Ni muhimu kuwa hizi rasilimali na fedha ambazo zitatoka katika kaunti hizi zigawanywe na kauti zipate pesa zake hapo hapo ndani na sheria ziweko ambazo zinaweza kustiri na kuhakikisha wenyeji wenyewe wanafaidika kwa mali hio. Kwa haya mengi, ninaomba kuunga Mswada huu mkono."
}