GET /api/v0.1/hansard/entries/262250/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 262250,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/262250/?format=api",
    "text_counter": 119,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mung’aro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 76,
        "legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
        "slug": "gideon-maitha"
    },
    "content": "Ahsante Bw. Naibu Spika wa Muda. Pia ninataka kuchukuwa fursa hii kumpongeza Waziri wa Serikali za Wilaya kwa Mswada huu ambao tunachangia. Mengi yameongewa lakini pia mimi nitachangia kidogo ijapokuwa mimi ni mwana kamati wa kamati ambao kuanzia kesho itajihusisha na washika dau hili kupata maoni zaidi juu ya Mswada huu ambao uko mbele yetu. Ningependa kuongezea kwamba kama tumeamua kuwa na serikali za ugatuzi na kwamba tunapeleka mamlaka mashinani, basi tusipeleke mamlaka nusu nusu. Lazima viongozi watakao chaguliwa kama Gavana na wale wengine wapewe uwezo kamili hili waweze kutatua matatizo ambayo yamekumba watu wa sehemu tofauti tofauti kutoka uhuru. Jambo lingine ambalo singesita na sitaona haya kulisema hapa, ijapokuwa ninajua jana ilikuwa hoja katika Jumba hili, sisi hasa watu wa Mkoa wa Pwani tunawasiwasi kwa hivyo tunaunga unga mkono kikamilifu kwamba kiongozi wa taifa atakae changuliwa katika siku sijazo awe ni kiongozi ambaye anaunga mkono Katiba hii. Hii ni kwa sababu sisi watu wa Pwani tunahistoria ya mwaka wa 1963, Kenya ilipata uhuru na serikali ya majimbo lakini kwa sababu majimbo hayo yalikuwa hayajakamilika kama haya ya sasa ambayo itakamilika 2015, wasiwasi ni kwamba tunaweza kurudishwa mwaka wa 1963 wakati ambapo marehemu Ronald Ngala na wenzake walienda kule Lancaster kupewa Katiba ya Majimbo lakini mwaka mmoja baadaye ikafutiliwa mbali na wakarudi pale pale kwa serikali moja ya Jamuhuri ya Kenya. Kwa hivyo ni muhimu kuelewa kwamba wale watakao kwenye nyadhifa mbali mbali hawatakuwa tu viongozi waliochaguliwa kwa ajili ya kazi zao lakini inapaswa wawe viongozi watakaotekeleza Katiba hii kikamilifu. Hilo ndilo litawaondoa Wakenya katika ugandamizi ambao umekuwa ukiendelea katika nchi hii. Kwa upande wa mapato, lazima iwe wazi kwamba asilimia fulani ya mapato kutoka sehemu tofauti tofauti ibakie katika sehemu hizo. Lazima jambo hilo liwekwe waz. Isiwe tu ni jambo la kufikiriwa. Lazima jambo hilo liwekwe katika mswada huu. Kwa mfano inafaa ijulikane kwamba katika eneo la pwani kuna utalii, madini, mabandari, na vilindi. Sote tuko Kenya moja lakini watu walioko Masai Mara, kwa mfano, wanaweza kupata asilimia fulani ya ushuru wa utalii ili hali kule pwani hakuna ushuru huo katika mahoteli na mbuga za wanyama kama vile Tsavo. Kwa hivyo lazima ielezwe wazi katika mswada huu kwamba kuna asilimia fulani ya mapato katika sehemu hizo ambayo itakusanywa kama ushuru. Nimesikia wenzangu wakijadili sana suala la bendera. Hawa magavana kutoka magatuzi yote 47 wanaweza kutumia bendera ya Kenya. Suala muhimu ambalo tungejadili ni lile la ushuru. Kila kaunti, ili tuweze kuhamasisha mambo ya usalama katika nchi, yapasa iwe na usajili wa nambari za magari yake. Tukifanya hivyo tutapunguza wizi wa magari na mambo mengine. Kwa hivyo sioni ugumu viongozi wote waliochaguliwa wakitumia bendera moja ya taifa. Mwisho, ili niweze kuwapa wenzangu nafasi, najua tutapata fursa ya kuongea na washika dau kuanzia kesho. Nikiwa mwanakamati nitaweza kuchangia mswada huu zaidi. Ningependa kusisitiza sana hili suala la serikali za mikoa hasa kuhusu wakuu wa wilaya na wakuu wa tarafa. Ikiwa wanataka kuandikwa kazi wasipelekwe tu na serikali kuu katika gatuzi hizi. Pawekwe mipango hivi kwamba kila gatuzi itenge nafasi zake na wapewe nafasi ya mbele hao wakuu wa wilaya na wakuu wa tarafa. Wakiandikwa kazi basi wawe chini ya magavana na kuchukuwa amri kutoka kwao wala siyo kutoka kwa serikali kuu. Kwa hayo machache, nashukuru. Nitachangia zaidi katika kongamano totakalokuwa nalo baina ya kamati yetu na washika dau wengine. Ahsante."
}