GET /api/v0.1/hansard/entries/262251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 262251,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/262251/?format=api",
"text_counter": 120,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Joho",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 30,
"legal_name": "Hassan Ali Joho",
"slug": "hassan-joho"
},
"content": "Ahsante sana Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii muhimu ya kuchangia katika kufuma serikali ya mashinani ya ugatuzi. Ningependa kujiunga na wenzangu kumpongeza Waziri mhusika kwa kusimama imara na ofisi yake kukaa kidete katika kutengeneza serikali hii muhimu. Jambo ambalo ningependa tuzingatie kama Bunge ni sisi kuwaunga mkono Wakenya. Hili jambo la serikali ya mashinani halikutoka kwetu bali limetoka katika mawazo ya Wakenya. Wamejiamulia kujitengenezea serikali inayoweza kutatua shida zao na uwezo wa kufikia serikali kwa karibu. Jambo ambalo ningependa tuzingitie ni marekebisho ambayo ni lazima yafanyike kupeana uwezo wa kiraslimali. Serikali yenye uwezo wa kirasmali ndiyo serikali yenye uwezo wa kudumu. Uhaba wa raslimali ni uhaba wa uwezo wa serikali. Ni muhimu tuangalie wakati tunapounda serikali hii ya ugatuzi tuwape magavana uwezo kamili wa kuendesha serikali. Mamlaka ya afisi ya gavana na County Assembly ni muhimu sana, yawe yatakuwa yenye kufana na kudumu. Ninasema hayo kwa sababu county ya Mombasa ni ya bahati kuwa na bandari katika county zote japo tunaomba kwamba kuwe na bandari zingine kama Lamu. Kwa sasa tuko na county ambayo ina uwezo wa kuendeleza biashara, viwanda, utalii na kadhalika. Lakini tunakuta kwamba ukiangalia mifano iliyoko sasa, tuko na bandari ambayo inageuza mamilioni ya dola. Lakini sasa hivi bandari iko na shida kubwa ya kuweza kuteremsha mali kwa haraka ili meli ziingie nyingi na biashara iwe kubwa. Ukiangalia kwa kina utaona sababu ni kwamba bandari inaweza kuwa na bidhaa ama kwa kimombo wanasema “adequate equipment” lakini hazitumiwi kwa kikamilifu. Ukitazama kwa kina utapata kwamba barabara ama reli zinazo lingania na bandari hazijawahi kuboreshwa na mikakati sambamba ya kuegeza bandari. Kwa hivyo utakuta kwamba bandari inashukisha mali lakini barabara ya kutoka kwa bandari na kuelekea katika maeneo ambayo mali inaenda haibadiliki. Haya ni kwa sababu wahusika katika serikali na uwezo wa kubadilisha na uwezo wa kutia rasli mali pahali ambapo patakuwa na mazao makubwa hawana. Kwa hivyo haitakuwa na haja tukitengeneza Serikali ya ugatuzi ambayo haina uwezo wa kujiamulia ni barabara gani na mipango gani ambayo itaweza kupeleka sera za fedha na za kimaendeleo sambamba. Katika Serikali za ugatuzi kwa maoni yangu ziwe na uwezo ya kuwa na ushindani halisi na county zingine. Yaani ugatuzi ulioko Mombasa katika hali ya kuendesha Serikali na kuleta uwezo kwa wananchi kwa mfano sisi tukiwa tunafungua bandari huru Mombasa tutaraji kwamba county ya Kilifi ifungue bandari ya utalii ili tuweze kushindana kifedha. Tukifanya hivyo nchi yote itaweza kuwa sambamba na kuendelea mbele. Kwa hivyo mimi naunga mkono Mswada huu lakini ningependa sana tuangalie marekebisho muhimu ya uwezo wa rasli mali. Mimi ni mmoja wa wanakamati na nina imani kwamba nitasimama imara na kungalia kwamba ugatuzi ambao unaletwa ni wa kufana na kudumu katika sera hii mpya na pia tusihadaiwa na siasa. Hata mimi nataka niungane na wale ambao wanasema kwamba ni muhimu kwa Wakenya na sisi wengine kupigia kura viongozi ambao wana imani kamili na Katika hii mpya na wataitekeleza. Kwa hayo machache ningependa kusema kwamba ninaunga mkono na ningependa tuangalie marekebisho tukiwa na uwazi wa roho na uwazi wa moyo ili tukamilisha kutengeneza serikali ya ugatuzi. Kwa hayo machache, nashukuru sana."
}