GET /api/v0.1/hansard/entries/262648/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 262648,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/262648/?format=api",
"text_counter": 394,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niunge mkono Mswada huu kuhusu kubuniwa kwa Serikali za Kaunti hapa nchi. Ningependa pia kutoa shukrani nyingi kwa Waziri kwa kuleta Mswada huu hapa Bungeni. Huu ni Mswada ambao umeratibiwa baada ya kuzingatia maoni na fikra za wananchi wote. Hata hivyo, kuna baadhi ya mambo ambayo ningependa kuyazungumzia kwa kina kirefu kwa sababu tunajua kila jambo lina uzuri na ubaya wake. Jambo la kwanza ni kuhusu uhusiano wa kaunti na kampuni za kibinafsi. Hapa inapendekezwa kuwa kaunti inaweza kuwa na ushirikiano na kampuni au mashirika ya kibinafsi. Wasiwasi wangu ni kuwa maofisa au wafanyakazi katika kaunti fulani wanaweza kuanzisha kampuni zao za kibinafsi ili wafanye biashara na kaunti hizo. Pia wanaweza kuingia mkataba na kaunti ya kuleta bidhaa na mambo mengi. Jambo hili linaweza kuendeleza ufisadi katika kaunti zetu. Kwa hiyo, ninamwomba Waziri afikirie juu ya jambo hili kwa makini."
}