GET /api/v0.1/hansard/entries/262649/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 262649,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/262649/?format=api",
"text_counter": 395,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Ukulingana na Kipengee cha Tatu cha Mswada huu, kaunti yenyewe inaweza kubuni kampuni yake kwa minajili ya kutoa huduma fulani kwa wananchi wake. Kipengee hiki kinaweza kutumiwa na gavana na maofisa wake ili waanzishe kampuni zao. Wakati mwingine utaona ya kwamba gavana anaweza kuwahimiza watu wake kubuni kampuni huko akiwaahidi kuwa kaunti yake itafanya biashara na wao. Tunajua ya kwamba sheria za wafanyakazi wa Serikali zinawanyima haki ya kufanya biashara na Serikali hata kama wana kampuni zao za kibinafsi. Hii ni kwa sababu matendo yao yataleta mvutano kazini. Ni lazima Waziri pamoja na Serikali kuwa macho na kuhakikisha kwamba watakaofanya kazi katika kaunti zetu wasikubaliwe kufanya bishara yoyote. Hii ni kwa sababu jambo hili litachangia sana katika ufisadi na uporaji wa mali ya wananchi mashinani. Kwa hivyo, ni lazima tuweke mikakati thabiti ya kuhakikisha gavana na watu wake hawataruhusiwa kufanya biashara na kaunti yao. Mimi huzunika sana nikiona ya kwamba baada ya pesa za umma kuibiwa tunaanzisha kamati ya kuchunguza. Hii ni kama kukimbiza upepo kwa sababau hatutapata pesa hizo. Kulingana na Mswada huu, Serikal za Kaunti zimepewa nguvu zaidi kuliko Bunge hili. Ikiwa kaunti itakuwa na gavana asiyemwaminifu, basi pesa za umma zitapotea na wananchi hawatapata huduma."
}