GET /api/v0.1/hansard/entries/262650/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 262650,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/262650/?format=api",
"text_counter": 396,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Jambo la tatu ni kuhusu kuteuliwa kwa Wabunge sita maalum wa Bunge la Kaunti hapa nchini. Ikiwa uteuzi huu hautafanywa ka njia mwafaka utaleta hali ya kuvuta ni kuvute. Wakiteuliwa mara moja, tena baadaye kutakuwa na mjadala wa kuangalia idadi kamili ya Wabunge maalum watakaoteuliwa. Wakati huu kuna malumbano makali kuhusu mipaka ya maeneo ya Bunge. Ripoti imetolewa na watu wengi hawajaridhika na mapendekezo yake. Kwa hiyo, ni lazima mambo haya ya mipaka ya uwakilishi Bungeni yafanywe kwa njia itakayoridhisha watu wote. Tusipofanya hivyo kutakuwa na malumbano makubwa na tutapoteza wakati na pesa kutafuta tena maoni ya wananchi. Haifa kuunda tena jopokazi ili kupata maoni ya wananchi juu ya ni nani anayestahili kuteuliwa kama Mbunge maalum. Hii ni kwa sababu hatuna wakati wa kufanya hivyo kati ya sasa na uchanguzi mkuu ujao. Ni miezi michache inayosalia kabla ya uchanguzi mkuu. Kwa hivyo, tuweke mikakati maalum kabla ya wakati huo."
}