GET /api/v0.1/hansard/entries/262652/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 262652,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/262652/?format=api",
    "text_counter": 398,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, Kaunti itakuwa kama Serikali, kwa sababu itakuwa na bendera, seal na labda hata wimbo wake maalum. Kaunti itapewa uhuru hata wa kukopa pesa. Hata hivyo, Mswada huu hauonyeshi wazi mamlaka haya yanafika wapi. Hata pesa zinaweza kukopwa kutoka kwa mtu binafsi kisha Kaunti inawekwa kwenye matatizo. Wanaweza kuonyesha kwamba wako na pesa, kumbe ni watu fulani ambao wameingia na kufanya ufisadi. Utaona kwamba hizo pesa ambazo zinakopwa labda hata haziendi kufanya kazi inayotakikana. Ni lazima kuwe na mikakati, kutoka nyanja za juu kuteremka chini, ili kuhakikisha kwamba wakati Kaunti inakopa pesa kuna mkataba."
}