GET /api/v0.1/hansard/entries/262654/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 262654,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/262654/?format=api",
    "text_counter": 400,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, kusema kuna sub-counties ambazo zitakuwa zinalingana na constituencies--- Kuweka tena sub-counties ni kuleta matatizo mengine. Hii ni kwa sababu constituency iko na Mbunge. Ukiongeza muwakilishi wa sub-county, ataleta matatizo. Hii ni kwa sababu sub-county yenyewe itakuwa na jopo lake na Mbunge pia atakuwa pale. Kwa hivyo, hii italeta matatizo. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo lingine linaloandamana na hilo ni kwamba itakuwa na vigumu sana kupata pesa na kufanya kazi, kwa sababu ya majopo yatakayoundwa. Zile tume na kamati ambazo zitakuwa ni karibu kumi. Je, hizi kumi zitakuwa zikifanya kazi gani kutoka pembe moja hadi ingine? Mambo haya yote yatakuwa yakiletewa Gavana mmoja. Je, ikiwa atakuwa akifanya kazi ya kusikiza madai na mambo yalizungumzwa na kamati hizi zote, kazi yake mwenyewe itafanyika lini? Kuangalia kazi ya kamati moja itahitaji masaa matatu au hata siku tatu. Bw. Naibu Spika wa Muda, Kaunti zitaamua ni kiasi gani cha pesa ambayo majopo hayo yatakuwa yakipata. Je, kama pesa zitatumika vile manispaa zinatumia pesa leo, nchi hii itapona lini? Badala ya kupeleka sheria mashinani ili iwasaidie wananchi, tutakuwa tunawafanya masikini kupitia sheria hizo. Hata hivi sasa tuna shida kwenye tume zilizowekwa na Serikali. Kuna matatizo kuhusu pesa ambazo wahudumu kwenye tume hizo wanajipatia na wanataka kuzichukua waende nazo."
}