GET /api/v0.1/hansard/entries/262655/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 262655,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/262655/?format=api",
"text_counter": 401,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, tatizo lingine ni kwamba serikali za kaunti hazijawekewa vipimo vya matumizi. Kwa mfano, haijabainishwa gavana katika kila kaunti atakuwa na gari moja ama magari mawili. Labda hilo ni jambo ambalo litafanyika baadaye. Shida ni kwamba iwapo hali hiyo haitashughulikiwa hivi sasa, magavana watajipatia madaraka watakayotaka. Utaona gavana akitaka kununuliwa Range-Rover yenye thamani ya Kshs 20 million, na kama magari saba hivi ya kumfuata nyuma kwenye misafara yake. Atataka naibu wa gavana pia awe na magari kama hayo kwa sababu hakuna kiwango cha matumizi ya pesa kilichowekwa. Watatumia pesa bila kujali na kuziweka kaunti kwenye shida. Watasema: “Tuleni leo. Watakaokuja kesho watatafuta namna yao ya kupata fedha.” Bw. Naibu Spika wa Muda, ninamwomba Waziri aweke kielelezo kwamba katika kila kaunti kutakuwa na gari moja la kaunti yenye cc zisizozidi kiwango fulani tusije tukajipata na matatizo ya kujaribu kukimbizana na upepo umepita mbele yetu. Vile vile, suala la muundo wa kamati ya kusimamia masuala ya ulinzi katika kaunti pia ni lazima lizingatiwe kusije kukawa watu wanasimamia viti vya gavana, wanaweka mambo yao na kuamua wanavyotaka. Suala hili lisiposhughulikiwa ipasavyo, utaona kwamba askari wameandikwa wengi hata kupita mapato ya kaunti yenyewe, kwa sababu watu watataka kutafutia watu wengine kazi. Tunataka kuona Waziri akisema kwamba askari wa kulinda kaunti watapatikana kutoka Serikali kuu. Bw. Naibu Spika wa Muda, jambo la mwisho ambalo ningependa kuzungumzia ni kuhusu wanaopewa nafasi ya kuongoza wengine. Hivi sasa tunazungumzia mambo ya kuchagua watu. Kuna shida moja. Leo hata wale wanaowania viti vya ugavana wanafanya kampeini za kutafuta kura. Kama gavana atakuwa akipigiwa kura, hali hiyo italeta matatizo mengi sana. Kaunti zitakuwa zikiongozwa na wanasiasa, na wanasiasa hao watatakiwa kutunza hela za umma. Mtu akiwa gavana, atataka kupigania urais baadaye. Kwa hivyo, utaona kwamba pesa za kaunti ndizo zitakazotumiwa kufanyia kampeini kule mashinani. Ikiwezekana, hiki ni kipengele kinachofaa kushughulikiwa upya. Ninasema hapa leo kwamba inafaa magavana wachunguzwe kama vile tunavyowafanyia majaji wetu ili tuweze kuwajua wao ni watu wa namna gani. Tutafaulu iwapo magavana hawatapigiwa kura bali watachunguzwa ili kubainisha tabia zao zilivyo na kuweza kufahamu walikofanya kazi ama walipata uongozi katika sehemu gani, kwa sababu hao ni watu watakaowania kusimamia serikali ndogo za kaunti."
}