GET /api/v0.1/hansard/entries/263072/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 263072,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/263072/?format=api",
"text_counter": 50,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister for Gender, Children and Social Development",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Kazi ambayo imefanywa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Serikali za Mitaa ni nzuri sana, haswa ile kazi aliyofanya kupitia kamati aliyoichagua, ambayo ilizunguka kote nchini na kusikiliza maoni ya wananchi. Tunapoanza shughuli ya serikali ya ugatuzi, na haswa tunapozingatia suala la maeneo ambapo kura zitapiwa wale ambao watakuwa wenye kuwakilisha watu kwenye serikali za ugatuzi, kuna jambo la muhimu ambalo ni lazima tulijadili. Kuna maeneo ya kaunti ambayo ni madogo, na ambayo hayana watu wengi, na haswa sana ukizingatia kwamba wakazi wa kaunti hizo wanatakiwa kupatiwa nafasi za kutosha kama wale wenzao ambao ni wengi. Ni matumaini yangu kuwa tutakapokuwa tunajadili Mswada huu katika awamu ya tatu, mapendekezo yetu yatazingatiwa hasa kuhusu Kipengee cha 27. Kipengee hiki kinahusu idadi ya maeneo yanayotakikana. Ni lazima tuseme kwa uwazi kuwa kila kaunti iwe na idadi fulani ya maeneo. Kwa mfano, tunaweza kusema kila kaunti, iwe na maeneo 15 ya chini ambapo watu watachagua waakilishi wao. Ni mapendekezo yangu kuwa maeneo hayo yasipungua kumi. Kupitia Mswada huu tunaonyesha tuko tayari kuwahudumia wananchi wetu kupitia Serikali za Mitaani. Tutakuwa na uongozi wa kisiasa mashinani. Ni kupitia uongozi kama huu ambapo wanyonge katika jamii zetu watapata huduma na haki zao kuheshimiwa. Kupitia Serikali za Ugatuzi, Gavana atahikikisha ya kwamba amewahusisha watu wote katika utawala wake. Atahakikisha ya kwamba wanyonge na wachache katika Kaunti wanapata haki yao na huduma kama watu wengine. Pia sauti zao zitatambulika kule mashinani. Ni kipengee ambacho kinasema ya kwamba ikiwa Gavana na waheshimiwa Wabunge wake watashindwa kutekeleza majukumu yao, basi watalazimishwa kung’atuka mamlakani na kuomba upya kura kwa wananchi. Hili ni jambo la kutia moyo sana kwa sababu watatoa huduma wakijua ya kwamba wakiwa wazembe watapokonywa mamlaka yao. Hapa mwananchi wa kawaida amepewe nguvu na sheria hii. Kwa hiyo, hakuna njia ya mkato kuhusu kutoa kutoa kwa huduma kwa wananchi. Ni lazima Gavana asimamie pesa za kaunti kwa makini sana na awe na stakabadhi za matumizi ya pesa za umma. Jambo ambalo ningependa tulitilie mkazo sana ni kipengee hiki kinachowapa Wabunge uwezo wa kumlazimisha Gavana ang’atuke mamlakani. Kipengee hiki kimefanya kuwa chepesi mno. Ikiwa Gavana ametoka jamii ndogo, basi kuna hatari kuwa Wabunge kutoka jamii kubwa katika Kaunti wanaweza kumfanyia njamaa ya kumtoa mamlakani. Ni lazima kipengee hiki kiwe na uzito na ungumu fulani. Ni lazima pawe na masharti magumu kabla ya Gavana kulazimishwa kujiuzulu. Kwa hivyo, ningependa hapa tutie mkazo kidogo ili vikwazo viwekwe isiwe ni rahisi sana kumtoa Gavana mamlakani. Ikiwa kipengee hiki kitabaki kama vile kilivyo sasa, basi Gavana hataweza kufanya kazi vizuri. Kila mara atakubana na siasa za duni ambapo itakuwa ni vigumu kwake kutoa huduma kwa wananchi. Sina mengi ya kusema kwa sasa. Nitakomea hapa na kumpongeza sana Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Serikali za Mitaa kwa kuwasilisha Mswada huu hapa Bungeni. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu."
}