GET /api/v0.1/hansard/entries/264321/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 264321,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/264321/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Rai",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Lands",
    "speaker": {
        "id": 203,
        "legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
        "slug": "samuel-rai"
    },
    "content": "Pengine Serikali italaumiwa kwa sababu ya muda wa mwaka mmoja na miezi minane ambayo imepita kwa kutoweza kuleta hii Miswada hapa. Lakini kumbukeni kwamba sheria ambazo zinahitajika kuletwa hapa ni sheria ambazo ni lazima tuhakikishe kwamba kila kitengo kimehusishwa ili kuhakikisha kwamba hatukumwacha mtu yeyote nyuma. Na kwa sababu tulikuwa tumechelewa na Kamati imekuja hapa na roho safi na kusema kwamba muda ambao pia wamepewa, wanahitaji wapewe zaidi, naona kwamba haitakuwa ni dhambi kupeana muda huo ili tupate kuhakikisha kwamba kila mtu amehusishwa. Hatutaki kufanya mambo kwa haraka. Matatizo ya ardhi yanayokumba watu wa Pwani ni mengi sana na tunahitaji tuwe na wakati wa kutambua moja baada ya moja, ili tuone kwamba sheria ambazo zitapitishwa zitakuwa ni muafaka na zitaweza kutuongoza kwa kipindi cha maisha yetu ambayo yamebakia. Kama kutoka mwaka wa 1901 tumekuwa tukiishi na hizi sheria ambazo ni zaidi ya karibu miaka 100 za kikoloni na tumeona yale madhara ambayo tumeyaona muda baada ya muda, na hasa kama tunakaribia kufanya uchaguzi, kwa nini turejelee makosa tena? Waswahili husema kufanya kosa si kosa, kurejelea kosa ndio makosa. Kwa sababu tumeombwa kwa nia safi, tupe muda tujaribu kuhakikisha kwamba kila mtu amehusishwa, naona kwamba ni swala la kuvumiliana na ni swala la kuelewana. Si swala la kunyosheana vidole vya lawama wakati kama huu. Kwa hivyo, naomba Hoja hii ikubalike na iwatosheleze Wakenya ili nafasi ipatikane."
}