GET /api/v0.1/hansard/entries/264327/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 264327,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/264327/?format=api",
"text_counter": 185,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister for Gender, Children and Social Development",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuunga mkono Hoja hii. Kama walivyozungumza wenzangu ni kwamba maswala ya ardhi ni maswala nyeti sana na haswa kwa Wakenya kwa ujumla. Sisi tunaotoka Taveta na Pwani kwa ujumla, tunatarajia ya kwamba hili Bunge linaloheshimika yaani Bunge la Kumi, tutaweza kuzungumzia maswala ya ardhi na hasa sheria za kutulinda kwenye maswala ya ardhi ili tuweze kuhakikisha kuwa Wakenya watatoka kwenye yale matatizo waliokuwa nayo kwa sababu ya shida nyingi zilizotuweka kwa sababu ya sheria za kikoloni. Kwa kawaida, sisi kwa sababu ya uraia wetu na hasa kama Wakenya, tumeshazoea ya kwamba mara kwa mara kwa sababu ya sheria nyingi zilizoko, tumeweza kuwapokonya watu ambao walikuwa wanatakikana kuwa na ardhi kwa sababu ya kutoelewa sheria nyingi zilizoko. Sioni haja ya sisi kukimbiza hizi sheria na kuzizungumzia kama hakuna muda wa kutosha. Wakenya wanatungojea pia turudi mashinani tuwaelezea haswa hizi sheria zina nini ili wakati tukikubaliana kupitisha, wawe wameelewa kuna nini. Kwa hayo machache naunga mkono."
}