GET /api/v0.1/hansard/entries/26434/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 26434,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/26434/?format=api",
"text_counter": 422,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, naomba kuunga mkono Mswada huu wa Sheria za Udhamini wa Hundi za Dharura za Kaunti. Katibu Mkuu amepewa mamlaka ambayo akiyatumia vibaya yanaweza kuathiri wenzake. Utawala uliopita ulidhihirisha jinsi mamlaka yanavyoweza kutumiwa vibaya. Kuna sehemu fulani za nchi zilizopendelewa na zikaendelea sana kuliko sehemu nyingine. Sehemu hizi hazikubaki nyuma kwa kuwa hazikuwa na rasilmali, bali ni kwa sababu ya watu fulani mamlakani walitumia vyeo vyao vibaya. Sehemu hizi zina rasilmali ambazo zinaweza kusaidia kaunti. Lakini ni ugawaji wa pesa katika nchi hii umekuwa na mapendeleo. Kwa hivyo, napendekeza kuwa kipengee hiki cha nne kibadilishwe ili kiangazie sana mamlaka haya. Mamlaka haya ni lazima yapunguzwe ili kila sehemu ipate haki yake. Ikiwa kaunti fulani itaomba mkopo kutoka shirika fulani la fedha, ni lazima Bunge hili liunge mkono mkopo huo. Mwisho, sio kila wakati kuwa kaunti ikiomba fedha au mkopo ni lazima idhihirishe uwezo wake wakulipa. Inaweza kuwa wakati huo kaunti haina uwezo wa kulipa mkopo huo lakini ina rasilmali ambazo zikitumiwa vizuri zinaweza kutumika kulipa mikopo hiyo. Kwa hivyo, ni muhimu katibu huyo aangalie hayo. Kwa hayo machache, ninaomba kuunga mkono."
}