GET /api/v0.1/hansard/entries/266370/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 266370,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/266370/?format=api",
    "text_counter": 305,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, mpaka sasa kuna matatizo ya shangazi wetu kupata vyeti vya kumiliki ardhi. Mwanamke anafiliwa ndani ya nyumba na kaka zake wanamfukuza. Akienda kwa chifu anaambiwa kwamba wanawake hawana haki ya kurithi ardhi. Tunajua kwamba Katiba inasema kila mtu ana haki ya kuwa na ardhi humu nchini. Ninamuunga mkono yule mheshimiwa aliyesema kwamba utakuwa katibu wa kwanza wa kutekeleza sheria hii."
}