GET /api/v0.1/hansard/entries/272949/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 272949,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/272949/?format=api",
    "text_counter": 295,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Mhe Naibu Spika, CDF imefaidi maeneo mengi sana ya ubunge katika nchi yote nzima; ukiangalia miradi mingi iliyotekelezwa, imetekelezwa na CDF. Hii ni fund ambayo, kusema kweli, imeeneza maendeleo nchi nzima. Shida amayo tunaiona hivi sasa ni kuwa hawa ndugu zetu ambao tunawachagua, ama tuwanapatia mamlaka ya kuweza kutuhudumia wameanza kuzembea kazi. Tunaomba kuwa huu uzembe ukome kwa sababu unafanya ombi lako la fedha lisitekelezwe mara moja; wakitaka stakabadhi hizi, unazipeleka; mara zimepotea; huzipati na miradi mingi katika maeneo mengi ya ubunge inakwama kwa sababu ya uzembe wa hawa maafisa. Naomba kwamba huu uzembe uishe ama upungue."
}