GET /api/v0.1/hansard/entries/27306/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 27306,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/27306/?format=api",
    "text_counter": 142,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Kwa hoja ya nidhamu, Bw. Naibu Spika. Mnamo Februari 22, niliuliza Taarifa kutoka kwa Waziri wa Mikoa na Usalama wa Ndani kuhusiana na kuzorota kwa usalama katika sehemu ya kaskazini mwa Bonde la Ufa ambako uvamizi ulifanyika katika mikahawa tofauti tofauti katika Mji wa Eldoret na watu wakauawa na wengine kupatikana kiholelaholela kando ya barabara katika sehemu ya Kitale. Tangu wakati huo hadi sasa, Taarifa hiyo haijaletwa Bungeni. Kuzorota kwa usalama umekita mizizi kwa sasa na uvamizi unafanyika kila wakati. Ningeomba umshurutishe Waziri mhusika atupatie Taarifa hiyo ambayo inaweza kuleta afueni kwa watu wengi ambao wanahofia maisha yao kutokana na uvamizi huo ambao unafanywa na makachero tofauti."
}