GET /api/v0.1/hansard/entries/273477/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 273477,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/273477/?format=api",
    "text_counter": 345,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ms. Leshomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Mimi pia ninaiunga mkono Hoja hii. Kwa kweli, hakuna mtu ambaye angefurahia kile kitendo ambacho kilitendeka kweny steji ya mabasi ya Machakos hapa mjini Nairobi. Maisha ya watu yanafaa kulindwa. Jambo la kushangaza ni kwamba kila kunapotokea jambo kama hili, tunalaumu wanamgambo wa kundi la Al Shabaab. Inafaa tuangalie hali hii ili kubainisha ni shida gani tulionayo. Hii ni mara ya nne mabomu kulipuka. Kila wakati inasemekana tu bomu limelipuliwa pale ama pale. Tunangonjea kitu gani kifanyike ndiyo tusikie uchungu? Ni watu wangapi watakufa ndiyo tusikie uchungu kama hatuwezi kusikia uchungu kufuatia vifo vya hao watu wachache? Ninaiomba Wizara ya Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani, kwa sababu Waziri Msaidizi yuko hapa, wahakikishe wanajua ni kitu gani kinachoendelea. Jambo kubwa litakuja kufanyika na tutashindwa tufanye nini. Bw. Naibu Spika wa Muda, mabomu yanalipuliwa kila siku. Hali hii siyo wizi wa mifugo unaofanyika miongoni mwa jamii za Wapokot, Wasamburu na Waborana. Haya ni mambo mengine. Hii ni Nairobi, na Nairobi ni ya Wakenya wote. Ukisikia watu wameumia Nairobi, utaona kwamba watu kutoka kila Kabila wameathirika. Kwa hivyo ninaiunga mkono Hoja hii na kusema kwamba jambo hili ni lazima liangaziwe zaidi kubainisha kinachoendelea. Hii ni kwa sababu tunaweza kungojea halafu jambo kubwa likafanyika, na haitakuwa vizuri kwa nchi hii. Ahsante, mheshimiwa, kwa kuileta Hoja hii Bungeni."
}