GET /api/v0.1/hansard/entries/273518/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 273518,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/273518/?format=api",
    "text_counter": 386,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, nilipokuwa nikija nilisikiliza mazungumzo haya kupitia Idhaa ya Kiswahili ya KBC. Mazungumzo haya yanatangazwa moja kwa moja na Wakenya wanahamaki sana ya kujua kilichofanya nchi hii kwenda kupigana katika nchi ya Somalia. Swali ni moja na Wakenya wanataka kujibiwa. Je, vita hivi vya sasa vinahusu nchi yetu ya Kenya vipi? Uwazi wa mambo ni kwamba Kenya ilidharauliwa. Kenya haina nia ya kuchukua hata inchi moja ya Somalia. Kenya haitaki kukaa katika nchi ya Somalia. Lakini madharau yaliingia katika nchi hii wakati maharamia walitoka kwao na kuingia katika nchi yetu kwa uwazi na madharau ambayo hayajaonekana. Walichukua mtalii na kutoroka naye. Walienda wakumuua na kurudi tena na kuchukua mtalii mwingine. Bw. Naibu Spika wa Muda, vijana walioko katika vita kupigania nchi yetu ni watoto wetu. Kwa nini wako katika mstari wa mbele vitani? Wako mbele ili kulinda taifa letu. Taifa hili halitalindwa na Mmarekani, Mhindi wala Mtanzania. Taifa hili litalindwa na Wakenya ambao ni watoto wa nchi hii waliozaliwa na akina mama na wazee wa nchi hii. Wale watoto wetu ambao wanapigana wanataka kusikia kwa sauti moja kwamba wanachokifanya kinaungwa mkono na Wakenya. Hii ni kwa sababu wako pale kutoa maisha yao. Katika vita hivyo, kuna vijana waliouwawa miaka miwili iliyopita na wengine hata hawana watoto. Kama watatusikia tukisema kwamba vile vita wanavyopigana havifai au ni vya kubahatisha, hawatakuwa na roho ya kujitolea. Kwa hivyo, ili wajitolee mhanga na kupigania nchi yetu, inafaa tutangaze wazi kwamba vita wanavyopigana ni kwa sababu ya kulinda nchi yetu. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuhusu mlipuko ulitokea katika uwanja wa mabasi, ningependa kusema kwamba Kenya sio nchi ya kwanza kwa mambo hayo kutokea. Kudharau na kutoona kwamba kikosi chetu cha polisi kinafanya kazi--- Nchi hii iko katika ramani ya ulimwengu. Mataifa yanayotuzunguka yanatuona sisi kama Marekani ya Afrika. Mtu anayetaka kuwa mwizi mwenye ujuzi sana anaingia katika taifa letu la Kenya. Je, ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu hapa ndipo utapata mali ya kuiba. Katika nchi zingine, hakuna kitu cha kuiba. Hata ukiiba bilioni moja ya pesa zao, ukibadilisha fedha hizo ni kama Dola 10,000 tu. Mtu akiiba billioni moja za Kenya, atakuwa amepata karibu Dola milioni moja. Katika nchi zingine, hakuna usalama kama nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo, mambo yanayotokea hapa sio kwa sababu ya kushindwa kwa polisi. Tunajua kuwa tunalindwa kutoka asubuhi hadi jioni. Tunajua taifa hili liko katika matata kutoka asubuhi mpaka kesho kutwa. Idara ya polisi imeweza kufanya kazi kwa sababu miaka nenda miaka rudi, ni mlipuko mmoja tu uliotokea hapa. Ninataka kuwaunga mkono polisi wetu na kusema kwamba majeshi yetu yafanye kazi na polisi na kuona kwamba mambo yanaenda vyema."
}