GET /api/v0.1/hansard/entries/27393/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 27393,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/27393/?format=api",
"text_counter": 229,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ms. Leshomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika. Ningependa kuunga mkono mambo ya kamati hii. Kitu cha muhimu ni mwananchi kupata huduma za Serikali karibu naye. Kamati hii itakuwa muhimu na itasaidia wananchi wote wa Kenya. Saa zingine, unaweza kupata kamati imeundwa lakini haiyajali masilahi ya wale walio mashinani. Kamati kama hizo hazijali watu walio mbali. Zinashughulikia watu wanaoishi sehemu kama vile Nairobi, Mombasa na Kisumu. Ukiangalia wananchi ambao wako katika sehemu za mashinani, ni watu waliotengwa. Ikiwa itasemekana kupata kazi katika kamati lazima mtu awe na digrii au Masters degree, je, Wakenya wote wamesoma mpaka wakafika viwango hivyo? Sio wote waliosoma. Wale watakaofaidika ni wale wamesoma kwa vile masomo yalifika sehemu wanazotoka zamani. Mambo ya kuchagua viongozi wa commission lazima yaangaliwe vizuri. Mtu akichaguliwa kama kiongozi, uongozi pia ni kipawa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mtu anakuwa kiongozi kwa sababu amepewa kipawa hicho na ana bidii katika roho yake. Watu wa mashinani watafungiwa tukisema lazima wawe na digrii, diploma ama Masters. Kuna watu ambao wamepewa vipawa vya uongozi na Mwenyezi Mungu. Kamati itakapoundwa, inafaa iwe na watu wa kutoka mashinani. Kamati hiyo inafaa iwahusishe Wakenya wote. Haifai kuwafungia wengine. Kusema ukweli, katika kuunda kamati hizo, kuna watu ambao hawahitajiki. Hebu angalia kamati zilizoundwa juzi, Kenya kuna makabila 42 lakini kamati nyingi hubuniwa na watu kutoka makabila matatu ama manne. Katiba hii inalinda Wakenya wote na tunataka iwalinde Wakenya wote. Kamati zisiwe zinamilikiwa na watu wa kabila moja. Tunataka Wakenya wote wajivunie mambo yaliyo Kenya yetu. Hatutaki watu wengine kuwekwa kando. Ni kama wengine hawastahili kupata hizo kazi. Hata wengine wakituma maombi yao, hawawezi kuwa shortlisted ili waweze kujitetea. Tulipitisha Katiba sisi wote. Ningesema kwamba mambo ya digrii yawekwe kando wakati wanachama wa kamati wanapochaguliwa. Ahsante kwa kunipa nafasi hii."
}