GET /api/v0.1/hansard/entries/27412/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 27412,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/27412/?format=api",
"text_counter": 248,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Namwamba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 108,
"legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
"slug": "ababu-namwamba"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ninakushukuru kwa fursa hii nichangie mjadala huu kuhusu hii sheria ya kubuni Tume hii. Kati ya Tume zote ambazo tumepata fursa ya kubuni chini ya hii Katiba mpya, hii ndiyo Tume ambayo tunaweza kuita Tume ya mwananchi wa kawaida. Hii ni Tume ya Mkenya wa kawaida. Tume hii itashughulikia masuala ya Mkenya wa kawaida katika sehemu mbalimbali za taifa hili, hasa kwenye sehemu za mashinani. Utakumbuka kwamba swala la Tume hii kutazamwa kama Tume ya mwananchi wa kawaida ni muhimu sana kwa sababu sasa tunaingia kwenye mfumo wa kusambaza mamlaka na rasilmali katika sehemu za mashinani katika taifa hili. Tunaposambaza mamlaka na rasilmali, vile vile tunasambaza uwezekano wa kuhujumu haki za mwananchi katika sehemu hizo. Ikumbukwe kuwa, Serikali za Maeneo ambazo zitasimamiwa na governors, zitakuwa na mamlaka yote ya kiserikali na jukumu la kuhudumia wananchi katika sehemu hizo. Kwa hivyo, ni lazima Bunge hili lijue ya kwamba tunaposambaza mamlaka ya kiasi hicho, ni lazima pia tuwe na mipangilio ya kulinda haki za mwananchi wa kawaida katika sehemu hizo ili tusije tukarudia historia mbaya ya kudhulumiwa kwa wananchi ambayo tumeshuhudia hapo mbeleni. Tumeona Utawala wa Mikoa katika taifa hili kwa muda mrefu sana ambao umekuwa utawala wa kidhalimu kabisa. Hii ndiyo sababu moja ya maswala ambayo wananchi walitaka yabadilishwe katika mabadiliko ya Katiba. Ilikuwa ni kubadilisha mfumo wa Utawala wa Mikoa. Kwa hivyo, Tume hii ni lazima vile vile tuipange kwa njia ambayo itaipa nafasi kuonekana na kuhudumu katika maeneo ya mashinani katika taifa hili. Kwa hivyo, ningependa kuunga mkono."
}