GET /api/v0.1/hansard/entries/27424/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 27424,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/27424/?format=api",
"text_counter": 260,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Namwamba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 108,
"legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
"slug": "ababu-namwamba"
},
"content": "Bw Naibu Spika, ninashukuru. Inafaa kufahamika kwamba tunatekeleza Katiba na tunabuni sheria ambazo zina umuhimu mkubwa. Ninaamini kwamba Bunge hili lina jukumu la kuhakikisha kwamba tunachukua muda wa kutosha ingawa tumo kwenye haraka, lakini ifahamike pia kuwa haraka haraka haina baraka. Mhe. Godhana anafahamu sana kuwa haraka haraka haina baraka. Ni muhimu sana Tume hii iweze kusambaa na tuweze kuiona na kuihisi katika sehemu zote za taifa hili ili wananchi kule mashinani ambao kila mara haki zao zinadhulumiwa waweze kupata nafuu kupitia kwa Tume hii. Ningependa kuunga mkono wale ambao wamependekeza kuwa afisi kuu ya Tume hii iwe katika sehemu moja ya mashinani katika taifa hili. Nimemsikia mhe. Mungatana akipendekeza afisi kuu ya Tume hii inaweza kuwa katika Pwani, hata kule Tana River; sehemu ambazo kwa kawaida, ukitazama historia ya taifa hili, zimesahaulika pakubwa. Tunafaa kufahamu kwamba tunapotekeleza Katiba hii tunavunja minyororo ya udhalimu wa miaka mingi na tunaanzisha mfumo mpya wa haki na usawa katika taifa hili. Bw. Naibu Spika, si kitambo sana katika taifa hili, kulikuwa na msemo kwamba, kuna haja gani kuharibu fedha kumtafuta wakili ikiwa unaweza kumnunua hakimu? Hayo ndiyo mambo ya kihistoria ambayo tunabadilisha kupitia masuala kama haya. Kwa hivyo, ningependa kusisitiza kwamba tuweze kuisambaza Tume hii ili wananchi katika sehemu mbalimbali za taifa hili waweze kuyahisi na kupata manufaa ya Tume hii. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}