GET /api/v0.1/hansard/entries/276594/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 276594,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/276594/?format=api",
"text_counter": 430,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba nitoe mchango wangu kulingana na makadirio ya ziada ambayo yamewasilishwa na Waziri wa Fedha. Bw. Naibu Spika wa Muda, nikiunga mkono Hoja hii, namuomba Waziri wa Fedha kusikiliza ushauri wetu kwa makini. Hii ni kwa sababu ana masikio lakini hataki kusikiliza ushauri wetu. Shida yao kubwa ni kuwa hawazingatii ushauri wowote. Tafadhali Bw. Waziri, fungua masikio yako leo. Bw. Naibu Spika wa Muda, Kamati ya Bunge ambayo inahusika na makadirio ilimshauri Waziri na kumuelekeza vile ambavyo ilionelea makadirio hayo ya fedha"
}