GET /api/v0.1/hansard/entries/276597/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 276597,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/276597/?format=api",
    "text_counter": 433,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "yawekwe ama yaelekezwe, lakini hawakusikia. Walikataa katakata na wakaja hapa Bungeni na kuendelea vile walivyokuwa wanataka. Ni nini kilichotokea? Walimu na madaktari wakagoma. Iliwabidi watafute pesa za ziada ambazo hazikuwa katika makadirio ili wapate kutimiza yale yale ambayo tulikuwa tumewaambia katika Kamati ya Fedha, Mipango na Biashara. Wakati huu tukikutana katika Kamati hiyo kuna mambo kadha wa kadha ambayo tutayachambua na kuyaleta hapa. Wakati huu, naomba Waziri wa Fedha ayasikie na kuyaweka maanani. Bw. Naibu Spika wa Muda, namshukuru Waziri wa Fedha kwa kuweka mkazo na kuhakikishia Bunge kuwa fedha za sehemu za uwakilishaji Bungeni, ambazo tunaziita, Constituencies Development Fund (CDF) na Local Authorities Transfer Fund (LATF) hazitaondolewa. Ninampa pongezi kwa kusema CDF itabaki vile ilivyo. Kama kuna matatizo ya vile pesa zinatumiwa, basi naomba aangalie mbinu mwafaka ya kusuluhisha matatizo hayo. Suluhu si kuondoa pesa hizi za CDF. Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba wakati huu pia muangalie mambo ya riba kwa sababu wananchi wanaumia. Hivi juzi benki zimeongeza riba kwa kiwango cha juu sana. Hakuna mtu anayeajibika. Mara nyingi mnazunguka hapa na pale mkisema kuwa riba hii itakuja chini ilhali benki nyingi hapa nchini zinatangaza faida kubwa sana ambazo si za kawaida. Ukipata benki inatangaza faida ya mabilioni ya pesa na sehemu zingine za uchumi hazipati hizo faida, basi utajua kuna tatizo fulani. Bila shaka kuna uporaji wa fedha. Ninamuomba Waziri aangalie benki hizi kwa makini sana kwa sababu sikubaliani nazo kuwa zinafanya biashara ya haki. Kuna pahali ambapo wanahujumu uchumi wetu. Nasikitika kwamba Waziri Ameacha kando Wizara ya Maji na tukiangalia Wizara hii ina upeo mkubwa sana katika uchumi huu. Katika makadirio haya Waziri, ameiacha. Naomba uyafikirie vile yalivyo."
}