GET /api/v0.1/hansard/entries/276598/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 276598,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/276598/?format=api",
    "text_counter": 434,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Naunga wenzangu mkono ambao wamesema kwamba mara nyingi Wizara ya Fedha huwa haisambizi fedha katika mikoa yote. Hata nikiangalia sioni kama mmepeana fedha kwa barabara ya Voi-Mwatate-Taveta na hivi sasa kazi yake inatarajiwa kukwama kwa sababu zile fedha mlikuwa mmeipatia katika makadirio yaliyopita zimeisha. Mwenye kandarasi mliomweka pia ameshindwa na kazi. Natumaini kwamba Waziri ambaye anahusika atachukua wadhifa wake vizuri na ahakikishe kuwa hiyo barabara imeisha ili angalau wakati huu wake, Waziri aambiwe na watu wa Pwani kwamba si yeye anawasukuma kwenda kwa Mombasa Republican Council kwa kutowapatia hela za kutosha. Mara nyingi nyinyi ndio mnawasukuma watu wa Pwani kwenda mrengo mwingine, kwa kukataa kuwapatia fedha za kufanya maendeleo katika mkoa wa Pwani. Natumai wakati huu utahakikisha kuwa watu wa Pwani wameangaliwa kikamilifu na barabara ya kutoka Voi kwenda Taveta imepatiwa pesa."
}