GET /api/v0.1/hansard/entries/277784/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 277784,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277784/?format=api",
"text_counter": 255,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Yakub",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 378,
"legal_name": "Sheikh Yakub Muhammad Dor",
"slug": "sheikh-dor"
},
"content": "Ahsante sana Bi. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ili nichangia hotuba ya mheshimiwa Rais kwa taifa letu la Kenya. Kwenye mambo ambayo ningependelea kuchangia ambayo Wakenya wataweza kujivunia kwa kazi aliyoifanya mheshimiwa Rais, ninafikiri ni machache kuliko mengi ambayo tunaweza kujivunia. Mojawapo ya yale mambo tunaweza kujivunia ni masuala ya Katiba mpya. Tunashukuru kwamba ni wakati wa mheshimiwa Rais Mwai Kibaki ambapo tumepata Katiba mpya. Tunamshukuru, pia, kwa kazi nzuri ya kuleta mfumo wa CDF. Lakini mengi ambayo hatuwezi kuyashukuru; mengi ambayo yamezungumzwa hususan maswala ya barabara, ukija kwetu Pwani utapata shida ni zile zile. Mpaka leo maeneo ya Lamu na Taita Taveta--- Barabara kuu ya kutoka Changamwe, Miritini kuja huku Nairobi ni mbaya mpaka sasa. Ukiangalia maswala ya elimu ya bure, ingawa mfumo ulikuwa na sera nzuri mpaka leo kuna watoto ambao hawaendi shule. Moja katika sababu kubwa ni kwa sababu wazazi wao hawana uwezo wa kuwanunulia vitabu. Bi Naibu Spika wa Muda, ingawa tumeambiwa kwamba hii sera ni ya elimu ya bure lakini vitabu havijaweza kupatikana kwa shule ambazo ni za Serikali. Haya ni mambo ambayo tunatarajia yangezungumziwa na inatakikana yafikiriwe kwenye miezi iliyobakia kwa sababu wengi katika wanafunzi ambao ni kutoka familia maskini, hawaendi shule ambazo ni za Serikali. Hii ni kwa sababu hawana vitabu ingawa tumeambiwa hii ni elimu ya bure. Pia, ningependa kugusia maswala ya Mombasa Republican Council (MRC). Kwa upande wa Serikali tunasikia mazungumzo ambayo yana tofauti mara nyingi. Mara utasikia Serikali ikisema kuwa wako tayari kukaa na kikundi cha MRC. Baadaye tunaambiwa kwamba Serikali haitaki kukaa na kikundi cha MRC. Umuhimu hapa ni kujua shida za MRC ni nini, au kwa nini MRC wakakuja na mfumo huu. Pili, MRC, haiwezi kukaa na Serikali kwa sababu Serikali imewaita wao ni kikundi haramu. Mpaka waweze kuondoa hilo jina la kwamba MRC ni kikundi haramu, ndio viongozi wa MRC watakuwa na moyo wa kukaa na Serikali. Sisi tunasema kama viongozi wa kutoka Pwani kwamba walichukulie hili jambo kwa utaratibu. Jambo la kwanza ambalo Serikali inafaa ifanye ni kuondoa kile kitengo kwamba MRC ni haramu; wakiondoe kwa haraka halafu mengine yaweze kuzungumzwa. Katika maswala ya uzalendo ambayo Mhe. Rais alizungumzia kwenye Hotuba yake, tumesikitika kuona kwamba huku tunaambiwa tuwe na uzalendo ambao ndio sheria na ndio sawa kwa sababu sote ni Wakenya na sisi sote nchi yetu ni moja, lakini wakati vikundi mbali mbali vinajikusanya kama Gikuyu, Embu na Meru (GEMA) au Kalenjin, Maasai, Turkana na Samburu (KAMATUSA) hatumsikii Rais akizungumzia kwamba vikundi kama hivyo vitaondoa uzalendo. Leo ni GEMA, kesho ni KAMATUSA kesho kutwa itakuwa ni maswala ya makabila mengine. Sisi tunataka Rais kwa siku ambazo amebakisha atuonyeshe kwa vitendo kwamba anataka uzalendo uwepo ndani ya nchi yetu. Moja ni kuondoa vikundi vya ukabila kwa haraka. Bi. Naibu Spika wa Muda, tumeambiwa kuna pesa za wazee ambao wamefika miaka 65. Kwetu katika County ya Mombasa ni wazee wachache sana ambao walipewa hizo pesa. Kwa nini Serikali au kitengo ambacho kinahusika na Wizara hiyo kimewapa wazee wachache ilihali kuna wazee wengi Pwani ambao wana miaka zaidi ya 65? Tunataka wizara ambayo inahusika na maswala ya pesa za wazee iweze kuangalia wazee wote Kenya nzima na hususan Pwani na Mombasa County ili wazee ambao wamefika miaka 65 waweze kupewa haki zao kama vile wengine wanavyopewa. Bi. Naibu Spika wa Muda, nikimalizia ninafikiri kuna jambo la muhimu sana kwamba sote kama viongozi, hasa viongozi wa Bunge la kumi ambao tumefanya kazi nzuri kwa kupitisha Miswada mingi ya Katiba mpya pia ni muhimu tuchunge yale mazungumzo ambayo tunazungumza kwenye hafla za raia kwa sababu huu ni mwaka mzito au ni mwaka ambao unaweza kuleta balaa hata zaidi ya mwaka wa 2007. Nikimalizia, nilitarajia Mhe. Rais wetu jana agusie yale mazungumzo yanayozungumzwa na America na Uingereza ya kwamba wananchi wao wasije Kenya kwa sababu hakuna amani Kenya na hakuna ulinzi. Ninafikiri huu ulikuwa wakati wa Mhe. Rais kueleza ulimwengu mzima kwamba kuna amani na ulinzi Kenya na watalii wowote wanaweza kuja na hakuna shida yoyote. Kwa hayo ninashukuru sana na ninaunga mkono. Asante sana."
}