GET /api/v0.1/hansard/entries/277797/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 277797,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277797/?format=api",
"text_counter": 268,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mung’aro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 76,
"legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
"slug": "gideon-maitha"
},
"content": "Ninashukuru Bi Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii pia nichangie Hotuba ya Rais ambayo ilitolewa jana. Kwanza, ninataka pia nipongeze kwa juhudi ambazo Rais amejaribu kufanya katika ujenzi wa miundo misingi, hasa barabara. Vile vile, nataka kuuliza kwa sababu wenzangu wamechangia, ni kwa nini barabara ambayo inashughulikia bandari yetu ya Mombasa, ambayo inaleta pesa nyingi katika uchumi wa hii inchi, inakuchukua masaa matano kutoka Nairobi mpaka Miritini na masaa hayo hayo kufika Mombasa mjini? Lingine ni barabara ya kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Moi mpaka mjini Mombasa, na kutoka Mombasa mjini kwenda Nyali, Malindi na kwingine."
}