GET /api/v0.1/hansard/entries/277799/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 277799,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277799/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mung’aro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 76,
"legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
"slug": "gideon-maitha"
},
"content": "Inachukua muda mrefu sana na hatujaona mikakati ya Serikali baada ya kuona umuhimu hasa katika uchumi wa utalii ambao umeidhibiti hii nchi katika miaka hii mitatu ya kifedha iliopita. Vile vile, kuna barabara nyingine muhimu katika sehemu ya Pwani kama vile barabara ya Voi-Taveta ambayo inaungana na nchi ya Tanzania. Tumesikia Waziri Msaidizi akiongea kuhusu Namanga na kwingine, lakini hatujasikia akigusia Pwani. Ukifika Malindi, utapata kuna barabara ile kuu ambayo ingefufua uchumi sana, hasa utalii katika County ya Kilifi; hii ni barabara ya kutoka Malindi, Kakoneni kwenda Salaget; pia kuna barabara ya ufuo wa bahari kutoka Watamu kwenda Malindi. Hizi barabara zingeweza kufungua uchimi kwa hali kubwa sana katika sehemu hii."
}