GET /api/v0.1/hansard/entries/277800/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 277800,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277800/?format=api",
"text_counter": 271,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mung’aro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 76,
"legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
"slug": "gideon-maitha"
},
"content": "Tunashukuru kwa ule mradi ambao umeanzishwa Lamu ili kufungua bandari ya Lamu. Cha kushangaza ni kwamba huu mradi wa Lamu umeanzishwa wakati watu fulani katika Serikali wamejipatia ardhi katika ile sehemu ya bandari. Wamejipatia rasilimali zote kando kando ya ile bandari kabla mradi huu kuanzishwa. Je, hii itawezesha kuleta utangamano wa wananchi wa sehemu ya Lamu na Pwani na wananchi wengine wa Kenya? Kama tunaongea kuhusu mambo ya amani katika hii nchi, hatukusikia Rais jana akiongea katika Hotuba kuhusu swala la mipaka. Tume ya Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) imeenda kuhamisha watu ambao wameweza kuishi pamoja kwa miaka zaidi ya 50, na leo wanapelekwa katika vijiji vingine. Je, hii itaweza kuleta amani wakati wa kura ijayo katika nchi yetu?"
}