GET /api/v0.1/hansard/entries/277802/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 277802,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277802/?format=api",
    "text_counter": 273,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mung’aro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 76,
        "legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
        "slug": "gideon-maitha"
    },
    "content": "Kuhusu swala la Mombasa Republican Council (MRC), nataka nieleweke vizuri. Ilitushangaza jana kwamba Rais alisimama na akataja MRC, ambayo ni baadhi ya makundi ambayo yanajaribu kujiunda katika hii nchi. Swala la KAMATUSA halikuwa muhimu kwa Rais kuliongelea. Swala la GEMA aliona si muhimu; lakini MRC ambalo leo ni kundi ambalo limekuwa katika midomo ya Wakenya na hata Serikali, aliona muhimu aongee. Kundi hili linakutana kila mara na Mkuu wa Mkoa. Limekutana na Waziri wa maswala ya ndani ya nchi na wamejadili mambo kadha wa kadha. Jambo linalotushangaza bali na lile la kujitenga kwa Pwani na ambalo si mjadala wa viongozi wa Pwani, nikiwa mmoja wao, ni kuwa maswala ambayo yanazungumziwa na MRC si mageni kwa Serikali hii. Kwa mfano, swala la ardhi katika Pwani ni swala nyeti. Ni swala ambalo limechukua miaka mingi kutatuliwa na Serikali yetu. Ni akina nani ambao wamejigawia ardhi ya Pwani, hasa ufuo wa bahari? Ni watu waliotumika katika Serikali zilizopita na Serikali ya sasa na wageni kutoka sehemu mbalimbali za dunia bila kutoa hata dururu moja. Ukichukua swala la uajiri wa wafanyakazi wa umma ambalo limezungumziwa sana na kundi la MRC, si swala geni kwa Wakenya kwa jumla na hasa Wapwani. Ni watu wangapi wa kutoka Pwani ambao wamefutwa kazi kwa muda wa miaka mitano iliyopita kutoka nyadhifa mbalimbali Serikali? Mmoja wao akiwa sasa ni mheshimiwa katika Bunge hili, Bw. Baya, Naomi Sidi, James Mure wa Kenya Ports Authority, Mkuu Wa Mkoa, Bw. Mwero, Zombo na wengine wengi? Hili ni swala ambalo kila mara watu wanajaribu kulisukuma chini ya meza. Kila mara tunaambiwa kuwa hakuna watu ambao wanaweza kufanya kazi hii au ile nyingine kutoka Pwani. Hiyo ni mifano ya baadhi ya watu kutoka Pwani waliotimuliwa kutoka Serikali hii na Serikali zilizopita."
}