GET /api/v0.1/hansard/entries/277803/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 277803,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277803/?format=api",
"text_counter": 274,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mung’aro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 76,
"legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
"slug": "gideon-maitha"
},
"content": "Swala lingine ambalo ni muhimu pia kwa watu kulijua ni kuwa Serikali hii haijakaa kitako na kuangalia kikundi cha MRC na viongozi wake ambao pengine hawajachaguliwa na wananchi wakichukua uwezo wa kuendesha shughuli za Pwani. Sisi kama viongozi waliochaguliwa tumejaribu sana. Miaka mitatu iliyopita, sisi kama Wabunge wa Pwani tulikutana na Rais wa Jamhuri hii na Waziri Mkuu na tukawaelezea maswala kuhusu ardhi, uajiri wa wafanyakazi katika mashirika ya umma na wizara mbablimbali za Serikali. Pia tuliongea kuhusu watu ambao wamefutwa kazi ambao wako na uwezo wa kufanya kazi. Lakini mfano mkubwa utaona hata leo katika magazeti kuwa Bw. Kijana Nyale kutoka Kilifi County aliajiriwa na tume ya kuajiri polisi na barua tofauti ikapelekwa kwa Waziri Mkuu na kwa Spika. Bado mnataka watu wa Pwani wasione kuwa hili ni tatizo ambalo ni lazima litatuliwe."
}