GET /api/v0.1/hansard/entries/277804/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 277804,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277804/?format=api",
    "text_counter": 275,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mung’aro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 76,
        "legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
        "slug": "gideon-maitha"
    },
    "content": "Ningependa kuihimiza Serikali na sisi kama viongozi wa Pwani tuongee na kuona tutajadili vipi swala la MRC. Tusije kuwalaumu kwamba wanasema Pwani si Kenya; pengine swala lao lingekuwa: Kwa nini Pwani si Kenya? Hii ni kwa sababu hawa watu wote ambao wameachishwa kazi Serikalini ni wakutoka Pwani, swala la ardhi na maswala haya mengine yote yanafanyika katika Mkoa wa Pwani. Tumeambiwa leo na hata Waziri mwenyewe amekubali leo kwamba barabara ya Namanga imetengenezwa, lakini aangalia Voi-Taveta Road. Hata ile barabara ambayo ilianzishwa mwaka jana, haina hata debe moja ya lami ambayo imemwagwa juu yake. Hayo ni maswala ambayo ni lazima Serikali iyaangalie kwa udani sana. Ni maswala ambayo ni lazima Serikali ijihusishe na viongozi badala ya watu kutoka Nairobi na kufikiria kwamba wanaweza kukaa Pwani. Sisi kama viongozi wa Pwani tumejaribu sana. Ningependa kuwauliza Mawaziri wanaozuru Pwani kujaribu kuongea na kundi hili la MRC. Siku moja nilijaribu kuwauliza viongozi wa Pwani tujaribu wote kutafuta suluhisho la swala hili la MRC. Hili ni swala ambalo tunahitajika kulizungumizia kwa makini sana. Utamsikia Waziri wa Utawala wa Mikoa na Usalama Wa Nchi amekutana na MRC peke yake na viongozi wa mkoa halafu akirudi anasema ni lazima tutatue swala hili. Swala hili tutalitatua tukiwa pamoja! Kwa mfano, Serikali inaweza kugawa ardhi yake kwa watu wa Pwani. Pia inaweza kutenga kiasi fulani cha pesa kwa minajili ya maendeleo ya watu wa Pwani. Si haki kwa sisi miaka nenda, miaka rudi, tunazungumza juu ya swala hili la ardhi bila kuwa na suluhisho la kudumu."
}