GET /api/v0.1/hansard/entries/277824/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 277824,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277824/?format=api",
    "text_counter": 295,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Joho",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Transport",
    "speaker": {
        "id": 30,
        "legal_name": "Hassan Ali Joho",
        "slug": "hassan-joho"
    },
    "content": "Jambo muhimu ambalo ningependa kusema ama ningetarajia kusikia likitiliwa shime na Mheshimiwa Rais hasa katika upande wa uchumi--- Kwanza, hata mimi ningependa kushikana na Mheshimiwa Rais kupongeza Wakenya na kuwashukuru katika uzalendo wao wa kulipa kodi, ili kufanya nchi yetu iwe ikijimudu kifedha na kuelekea na sera ya kujitegemea ili badaye tuweke kando pesa za ufadhili katika siku za usoni. Mheshimwia Naibu Spika wa Muda, kitu muhimu ambacho ningependa kuona kimezungumzia na Rais hasa ni katika fedha ambazo benki zetu zinalipisha katika mikopo - yaani rates za interest katika benki zetu. Ni kitu muhimu sana kuweza kupatia nafasi Wakenya kuendeleza biashara. Wazungumzaji waliokuwa mbele yetu wamesema kwamba kuna hatari ya watu kumezwa kifedha katika mienendo ya kifedha katika sekta ya benki na kadhalika. Kwa hivyo, Serikali ina majukumu ya kuangalia kwamba imelinda biashara za mkenya pale alipo, na kuweza kuwezesha Wakenya wengi kupata nafasi ya kujenga nchi kiuchumi na kupata mikopo katika benki zetu. Kitu muhimu ningependa kusikia katika Hotuba hii ni kuleta umoja ya Wakenya kwa niaba ya kuishi pamoja."
}