GET /api/v0.1/hansard/entries/277825/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 277825,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277825/?format=api",
"text_counter": 296,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Joho",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Transport",
"speaker": {
"id": 30,
"legal_name": "Hassan Ali Joho",
"slug": "hassan-joho"
},
"content": "Jambo muhimu ambalo Mheshimiwa Mung’aro na Mheshimiwa Nkaisserry walisema ni kwamba ukimwona Mkenya anaweza hata kutoka kwa runinga, kwa mfano MRC, na aseme yale anasema, ujue ni kuchoshwa. Ya kwamba pengine amevumilia kiwango mpaka sasa anasema: “Lile litakalokuwa na liwe.” Mimi ni mmoja wa wale ambao wanasema Pwani ni Kenya. Na ningependa Pwani iendelee kuwa Kenya bila kufikiria hata mara mbili. Lakini kitu cha muhimu ni kwamba tunataka kuona - na hili silo jambo jipya--- Ni jambo ambalo viongozi waliopigiwa kura Pwani, mwaka 2008 walikaa na Mheshimiwa Rais na wakamweleza zile issues ambazo zingali donda sugu katika maeneo ya Pwani. Issues hizo ndizo ambazo zinatumiwa na viongozi wa MRC, kama vile ardhi, barabara, ajira na kadhalika. Kitu cha kupewa kipaumbele ni kwamba watu wazungumze. Watu wazungumze, tuelezane. Ningechukua nafasi hii kusihi Mkenya yeyote pale alipo kwamba mambo ni mawili. Kama wewe ni mkenya pale ulipo, utambue ukenya wako. Hata ndugu zangu wa MRC nataka kwanza watambue wao ni wakenya. Kwa sababu ukitazama Mheshimiwa Naibu wa Spika wa Muda----"
}