GET /api/v0.1/hansard/entries/277830/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 277830,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277830/?format=api",
    "text_counter": 301,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Joho",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Transport",
    "speaker": {
        "id": 30,
        "legal_name": "Hassan Ali Joho",
        "slug": "hassan-joho"
    },
    "content": "Kitu muhimu ni kwamba zile shida ambazo zinawapata watu – na mimi nimepata nafasi ya kutembea karibu nchi hii yote; shida zipo, lakini Serikali izungumzie namna--- Jana wakati Raisi alisema kwamba Pwani ni Kenya, mimi nilimuunga mkono kwamba Pwani ni Kenya. Ningependelea aendelee kusema kwamba zile shida za watu wa Pwani pia tutaziangalia na kuzipa kipaumbele, ndio Mkenya popote alipo, ajisikie kuwa yeye ni Mkenya. Si lazima atoke Thika Road peke yake; hata yule wa kutoka Miritini, kwa sababu ni wazi. Mimi ningependa kumuunga mkono Bw. Mung’aro kwamba pahali pa kutega uchumi kama Bandari ya Mombasa--- Niashukuru Wizara ya Uchukuzi pamoja na Bandari sasa imeingilia mradi mkubwa wa kupanua Bandari ya Mombasa. Lakini pia tunasema ile barabara ambayo ingeweza kusaidia usafirishaji ili kuwezesha Bandari ya Mombasa kufanya kazi kwa wepesi pia nayo iangaliwe. Hii ni barabara ya kutoka Miritini had nje ya Mombasa. Hili ni jambo ambalo Serikali inafaa ilifanye. Hakuna mahali dunia hii ambapo mpaka leo wanafikiria kujenga barabara ya leni moja. Kila mtu akipanga kujenga barabara ndogo kabisa ni barabara ya leni mbili; yaani inapita magari mawili wakati mmoja. Kwa hivyo, tunataka kwamba Serikali ianze sera ya kujenga barabara. Ukianza barabara mpya, ile ndogo kabisa iwe ni barabara ya kupita magari mawili."
}