GET /api/v0.1/hansard/entries/277831/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 277831,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277831/?format=api",
    "text_counter": 302,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Joho",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Transport",
    "speaker": {
        "id": 30,
        "legal_name": "Hassan Ali Joho",
        "slug": "hassan-joho"
    },
    "content": "Bi Naibu Spika wa Muda, jambo lingine ambalo Raisi alizungumzia jana, na ningependa kusema kwamba ni muhimu, ni kuwa Serikali inayokuja iwe na msimamo imara kuhusu pesa za Constituencies Development Fund (CDF); pesa hizi ni asilimia mbili nukta tano, lakini zimeonekana zaidi kuliko zile zingine ambazo hubaki katika mfuko mkuu wa Serikali. Ukiingia katika maeneo ambayo hata hayako katika miji mikubwa, utaona miradi ya CDF; lakini ni nadra sana kuona miradi ya Serikali kuu. Kuhusu barabara au miundo msingi, infrastructure, ni muhimu iangaliwe na ifunguliwe. Utakubaliana na mimi kwamba utalii unaleta karibu Ksh98 billion katika nchi hii, na bado hatujaona maeneo ambayo yanasaidia utalii kusonga mbele yakiangaliwa kwa njia ambayo inastahili. Tunataka tuwe na daraja moja au mbili zaidi za kuvuka kutoka Mji wa Mombasa kuelekea kusini mwa Mombasa na kwingineko."
}