GET /api/v0.1/hansard/entries/277832/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 277832,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/277832/?format=api",
    "text_counter": 303,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Joho",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Transport",
    "speaker": {
        "id": 30,
        "legal_name": "Hassan Ali Joho",
        "slug": "hassan-joho"
    },
    "content": "Bi Naibu Spika wa Muda, jambo muhimu ambalo mhe. Rais amelizungumzia katika Hotuba yake na ningependa waheshimiwa Wabunge na viongozi wingine kuliendeleza ni swala la usalama wa nchi yetu. Ninapenda sana kulishukuru jeshi letu la Kenya kwa kazi nzuri ya kulinda mipaka yetu na hasa vita vyao dhidi ya magaidi katika nchi ya Somalia. Ni kupitia juhudu zao usalama wa Wakenya wote utapatikana. Ningependa kumpongeza mhe. Rais juu ya msimamo wake kuhusu uchaguzi ujao. Yeye angependa kuona uchaguzi wa haki na amani. Msimamo wake ningependa sisi viongozi tuufuate ili kuwe na amani katika nchi yetu. Ninampongeza kwa kusema kwa uwazi yuko tayari kumkabidhi mamlaka kiongozi yeyote atakayechaguliwa kwa njia ya haki na amani. Hili ni jambo nzuri. Kwa hivyo, ningependa viongozi wote kumuunga mkono mhe. Rais na tuwe tayari kuwapa Wakenya fursa ya kuchagua viongozi wawapendao kwa njia ya amani na haki. Kenya kama taifa ni kubwa zaidi kuliko sisi sote viongozi na hata mhe. Rais and mhe. Waziri Mkuu."
}