GET /api/v0.1/hansard/entries/280716/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 280716,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/280716/?format=api",
    "text_counter": 367,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba nami nichukue nafasi hii kutoa mchango wangu juu ya Hotuba ya Rais. Kwanza, ningependa kumpongeza Rais kwa Hotuba yake aliyoitoa hapa Bungeni. Ni Hotuba ambayo iliangazia mengi kuhusu maendeleo ya nchi hii. Nikimshukuru Rais kwa yote aliyosema, hata hivyo nina mambo mawili au matatu ambayo naomba yapewe kipaombele. Kwanza ni kuhusu uchumi wetu. Hali ya uchumi wetu unaendelea kuzoroteka. Lakini Rais hakutaja kipengele chochote kuhusu mikakati inayowekwa na Serikali ili kuboresha maisha ya wananchi. Hivi sasa, wananchi wameadhirika sana. Ningependa kuona mikakati ambayo itawasaidia wananchi wasiadhirike zaidi kuliko walivyoadhirika sasa."
}