GET /api/v0.1/hansard/entries/280717/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 280717,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/280717/?format=api",
"text_counter": 368,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mheshimiwa Rais aligusia ukarabati wa barabara. Alisema kuwa Serikali itaendelea kuzingatia sera za kuboresha barabara hapa nchini na hasa sehemu ambazo zina manufaa zaidi. Swali langu ni hili: Ni sehemu zipi ambazo hazina manufaa? Hata kule tulikuwa tunaambiwa zamani hakukuwa na manufaa na ambapo kulikuwa kumeachwa nyuma kimaendeleo, sasa mafuta yamepatikana. Barabara za huko ni mbaya sana. Hamna barabara zozote ambazo zimekarabatiwa ama kuwekwa lami. Je, hayo mafuta mtayatoa namna gani kutoka kaunti hiyo? Barabara nyingi katika Mkoa wa Pwani ni mbaya sana. Kwa mfano, barabara ya kutoka Voi kwenda Mwatate/Wundanyi ni mbaya sana. Imepewa kampuni ambayo imeshindwa kufanya kazi kwa haraka. Kampuni hii imekuwa pale kwa zaidi ya miezi 11 na imefanya theluthi kumi ya barabara hiyo. Huo ni uzembe wa hali ya juu. Kampuni hii haiwezi kazi hiyo. Wakati umefika sasa Serikali kukatisha kandarasi hiyo na ipewe kampuni nyingine ambayo itafanya kazi kwa haraka. Barabara ya kutoka Ndii kwenda Mgamboni kupitia Nyache ni mbaya sana. Je, barabara hii itagharimu Serikali kiasi gani cha pesa kukarabatiwa? Hakuna pesa ambazo zimetengwa kuikarabati katika Bajeti ya mwaka huu. Maafisa wa Serikali wanajaribu kubaini kiwango cha pesa ambazo zitahitajika kuirekebisha. Barabara hii itawasaidia watu wa Mgamboni kupeleka mboga zao Mombasa bila tatizo lolote. Lakini ufisadi katika Wizara ya Barabara ni mwingi mno. Tunaomba ufisadi huu uchunguzwe ili wanaopewa kandarasi hizi wawe ni watu wamebainika wazi wazi kuwa wanaimudu kazi hiyo ya ukarabati wa barabara hii. Barabara ya kutoka Voi hadi Taveta haijawahi kutengewa pesa zozote. Tunaambiwa kuwa bado maafisa wa Serikali wanafanya upelelezi kujua itagharimu pesa kiasi gani. Watafanya upelelezi huu hadi lini? Mpaka leo, tunaambia African Development Bank (ADB) ndio itatoa pesa za kujenga barabara hii. Ninaomba kama itawezekana kandarasi hiyo itolewe kabla ya mwisho wa mwezi wa Agosti. Tunaomba pesa hizi ziwekwe katika Bajeti ya mwaka huu itakayoanza mwezi wa Juni. Tetezi kule mashinani ni kuwa Serikali inaona ugumu kuweka barabara ya Voi/Mwatate/Taveta lami kwa sababu zile mboga zitakazo toka pale ni nyingi mno; zitafurika Mombasa na mboga za Mkoa wa Kati hazitakuwa na soko kule Mombasa. Kwa hivyo, Serikali inaendelea kudidimiza watu wa Taita au Mkoa wa Pwani kwa ujumla. Hilo tunalikataa! Tunasema wakati umefika usawa uwepo."
}