GET /api/v0.1/hansard/entries/280720/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 280720,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/280720/?format=api",
    "text_counter": 371,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, Rais alisema anataka usawa wa nchi. Ninamuunga mkono hapa. Tunataka usawa na umoja wa nchi. Wananchi wote washirikiane, kazi ziwe zinapeanwa kwa usawa. Juzi, tuliambiwa kuwa ukabila umekita mizizi katika vyuo vikuu. Watu wa jamii fulani ndio wameajriwa sana. Huu ni ukweli kwa sababu hivi juzi Waziri wa Uchukuzi analiunda Bodi ya Kenya Ports Authority (KPA). Aliweka watu wa jamii moja. Tunaenda wapi kama Waziri anaweza kuweka watu kutoka jamii moja katika Bodi ya KPA jamii moja? Je, watu wa Pwani hawana mtu hata mmoja ambaye amesomea uanasheria? Hawana mtu anayetosha kuwa katika bodi hiyo? Tunaambiwa wengine waliwekwa huko kwa sababu ya kazi zao Serikalini. Majukumu gani? Huo ni ukabila wa hali ya juu. Mimi kama Mbunge wa Mkoa wa Pwani, naushtumu kabisa na hatutakubali uendelee. La hasha! Mnataka watu wa Pwani waende wapi? Ikiwa hatuko pamoja, basi mtwaambie tuko wapi. Kwa nini mnatusukuma ukingoni? Tukisema hatuwataki, mtaanza kusema hawa ni wakabila lakini nyinyi wenyewe ndio mnatusukuma. Tunaambia Serikali iache ufedhuli!"
}