GET /api/v0.1/hansard/entries/280722/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 280722,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/280722/?format=api",
"text_counter": 373,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Tunataka kujua kwa nini pesa za mbuga ya Tsavo zinachukuliwa na Serikali kuu. Wale watu ambao wako katika maeneo ya mbuga, ni faida gani wanayoipata. Wao ndio wanashughulika kuangalia kuwa wale wanyama wanawalinda vilivyo. Na Bw. Spika wa Muda, nashukuru kuwa katika eneo la Bunge unaloakilisha, tunapakana nawe. Hawa wanyama pia wanakuadhiri. Nina furaha kuwa tutakuwa na Serikali ya Ugatuzi. Huu ugatuzi hautakuwa na maana kama wananchi wenyewe ikiwa hawatafaidika na rasilimali zao. Namshukuru mwenzangu, mhe. Mbunge alitangulia kabla yangu. Amegusia jambo la madini kuwa hivi sasa zile sera zilizoko za ugawaji wa fedha za madini hazisaidii wenyeji. Lililoko hivi sasa ni kuwa ukishapeana kibali cha mtu kuchimba maadini, umeagana naye. Atachimba kila kitu na kwenda nacho, hashurutishwi kuwasaidia watu pale maadini yanatoka kuwajengea shule, maji au hospitali. Ni abebe madini na aende. Je, wenyeji watafanya nini? Haya ndio matatizo ambayo yaliyotokea Nigeria walipopata mafuta. Wenyeji hawapati chochote. Ninashukuru tumepata mafuta Turkana. Tukiendelea na sera hizo, mtawaona Waturkana wakiendelea kuwa walivyo, na mafuta yote yataletwa Nairobi na Mabepari wa hapa Nairobi ndio watakuwa wanafaidika na hayo mafuta. Waturkana hawatakuwa na chochote. Wataita sasa wana madini mengi ambayo yametajirisha watu. Lakini, je, Wataita wanasemaje kuhusu madini hayo? Hamna chochote wanachopata. Hii ndio maana tunasema sera hizi zigeuzwe ili angalau watu wafaidike. Bw. Naibu Spika wa Muda, mwisho, ningependa kuongea kuhusu reli na uchukuzi. Hivi sasa, barabara ya kutoka Mombasa kupitia Nairobi hadi Kampala inatumika na malori makubwa tena mazito yaliyobeba makasha au mizigo. Hii ni kwa sababu uchukuzi wa reli umeachwa ufe ili hawa mabepari waendelee kuharibu barabara na kubeba makasha kwa kutumia malori yao makubwa makubwa. Kwa nini hatutumii reli? Ajali zinazotokea katikati ya Mombasa na Nairobi ni nyingi mno kwa sababu tunatumia barabara kusafirisha makasha. Kwa nini tusitumie reli? Hata ninashangaa kwamba reli ya kutoka Voi kwenda Taveta imeachwa ikafa. Watu wanaibeba kama"
}