GET /api/v0.1/hansard/entries/280724/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 280724,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/280724/?format=api",
    "text_counter": 375,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Ninashukuru Waziri yuko hapa. Ninatoa mchango wangu uje uone ile reli jinsi mlivyoiacha. Ni mali ya umma na ni mali ya Serikali lakini hakuna mtu ambaye anaiangalia. Imeachwa, watu wafanye wanavyotaka kufanya, wabebe hivyo vyuma na waende waviyeyushe ili wafanye navyo shughuli nyingine. Je, ni nani anayehusika? Hii ni reli ambayo inaweza kutumika kuunganisha Kenya na Tanzania ili tuokoe uchumi wetu. Nikimalizia, jambo la kusikitisha ni kuwa tuna vyuo vikuu vingi ambavyo vimeanzishwa. Lakini katika Mkoa wa Pwani, hatuna hata kimoja ambacho kimesajiliwa sawasawa. Tunazo zile zinaitwa “ constituent colleges” lakini hatuna chuo hata kimoja ambacho kimepewa mamlaka yote katika Mkoa wa Pwani. Inamaanisha nini? Ile kasumba mliokuwa nayo ya ukoloni mamboleo kwamba tuwe tunawaacha watu wa Pwani bado mnayo. Tunaomba mgeuke. Kama ugatuzi hautawageuza sijui ni nani. Labda ni wakati Yesu atarudi. Kwa hayo mengi, ninaomba niweke tamati."
}