GET /api/v0.1/hansard/entries/281549/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 281549,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/281549/?format=api",
"text_counter": 415,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Machage",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Roads",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": " Madam Naibu Spika wa Muda, shukrani kwa kunipa nafasi hii ili kuunga Mswada ulio mbele yetu mkono. Wakati wa kielelezo cha Katiba, kabla ya kupiga kura, wegine wetu walikuwa na mafikirio ya kuweka wakfu wa Miswada kadhaa ya kutekeleza Katiba kwa sababu wakati haukutosha. Haya mambo yaliingia kwa vichwa kiziwi na hayakusikilizwa. Sasa majuto ni mjukuu. Tuanza kuyaona sasa. Lakini basi wote tukakubali na tukakula kiapo kwamba Katiba iliyoko tutaitukuza na kuikubali na kuitekeleza vile ilivyo. Huo ndio wajibu wetu tuliyonao sasa; kwamba vipengele vyote vya Katiba vilivyoko ambavyo tulivipitisha kwa wingi wa kura za wananchi wa Kenya, vitekelezwe."
}