GET /api/v0.1/hansard/entries/281569/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 281569,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/281569/?format=api",
    "text_counter": 435,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kambi",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Medical Services",
    "speaker": {
        "id": 39,
        "legal_name": "Samuel Kazungu Kambi",
        "slug": "samuel-kambi"
    },
    "content": " Ahsante Bi. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa wakati huu. Naunga Hoja hii mkono kwa sababu kama Bunge, tulipatiwa uwezo na wananchi na Katiba tulioipitisha. Hatukupitisha Katiba ndio iwe kubwa kushinda wananchi. Tuko hapa kutekeleza matakwa ya wananchi na ndio maana inabidi tukiona pale ambapo kulikuwa kombo, turekebishe. Ningependa kusema hivi: Rais bado ana mamlaka ya kupitisha kile ambacho anaona kitafaa Wakenya. Siyo kupitisha kitu ambacho kitatuletea shida. Hii ndio maana, kwa hekima zake, aliona Mswada huu urudishwe kwetu ili tupitishe Mswada ambao utaleta manufaa kwa wananchi wa Kenya. Ndio maana umeletwa kwetu ili tuangalia vile vile, kwa hekima zetu, kama viongozi. Taifa nzima linaangalia ule mwenendo tunaenda. Ndio maana mimi nasema kuwa Mswada huu ni muhimu haswa ukiangalia unaguza sehemu nyeti ya ugatuzi. Ugatuzi ndio tumepigania kuanzia wakati tulipopata Uhuru. Tulikuwa na ugatuzi wakati huo. Lakini sheria zilizokuepo hazikuwa nzuri, mwafaka na za kudumu. Ndio maana zilibadilishwa na tukaenda kwa mufumo ambao wananchi wameukataa saa hii. Vile vile, hatuwezi kuendesha nchi bila fedha. Kwa hivyo, ni muhimu tupatiane muda huu ili tuyajadili kinagaubaga maswala haya ambayo ni nyeti na yameleta matatizo. Tufanye hivyo ili tuweze kuyapitisha kwa jumla na tuweze kuwahusisha wananchi ambao ndio nguzo muhimu ya nchi hii na uchumi wetu. Kwa hayo machache, naunga mkono. Ningeomba wale Wabunge wote wako hapa waangalie masilahi ya wananchi kwa sababu nafikiria kwamba walituleta hapa tuangalie masilahi yao."
}