GET /api/v0.1/hansard/entries/282069/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 282069,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/282069/?format=api",
"text_counter": 468,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, tukisema tunataka umoja wa taifa na tunataka kuunda taifa ambalo msingi wake ni wa utaifa wa Kenya, ningeomba vyama vizingatie sana viongozi wake wanatoka ukoo fulani. Kwa sababu ukiangalia kama Mkoa wa Kaskazini hivi sasa, hauna viongozi wa vyama. Kwa hivyo, utaona kwamba mwenyekiti akiketi chini kuamua ni nani atachaguliwa, anaangalia ukoo wake. Basi wengine hawatakuwa na nafasi. Wakati tunaanza kutafuta viongozi, hao watu wataingia tu kusindikiza wale ambao wanajiita jamii kubwa na wanajiita majina yanayofanana na uongozi wa chama. Lakini wale wachache bado wataendelea kufinywa. Ukiangalia upande wa Turkana, hakuna kiongozi wa chama. Kwa hivyo kama mwenyekiti wa kuchagua ni kiongozi wa chama, basi hawa watu hawana nafasi kutokea katika uongozi wa taifa. Kwa hivyo, nataka kutoa mwito nao wawe macho, wakubali na kuamua kwamba watafanya maamuzi kwa misingi inayozingatiwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa sababu Hoja hii imechangiwa na wengi, nataka kukoma hapo na kusema kwamba itakuwa ni dhahiri na jambo la maana kumuita Mwenyekiti wa Kamati kujibu na kufunga."
}