GET /api/v0.1/hansard/entries/283187/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 283187,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/283187/?format=api",
    "text_counter": 266,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Machage",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Roads",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": " Bw. Spika, nakushukuru kwa nafasi hii ili niunge mkono Mswada uliopendekezwa kwetu na Mkuu wa Sheria; Mswada wa marekebisho ya sheria za ziada kutoka siku 14 hadi siku 8. Mapendekezo ambayo ameyatoa kuunga huu Mswada ni kama vile kurekebisha sheria ambazo zina dosari kama vile sheria ambazo zinaangalia kazi yake ofisini, kutoa mamlaka kwa kazi yake na ile ya Mkuu wa Mashtaka. Sheria kama zile za kupendekeza kuongeza mahakimu kwa korti zetu na hata sheria za uchaguzi. Naona ni jambo la maana kwamba tukubali, kusudi zile sheria za ziada zipitishwe na kufanya Serikali iendeshwe vizuri. Hakuna sababu ya kukataa kuunga huu Mswada. Naomba wenzangu kwamba tuunge huu Mswada kwa dhati, kusudi Mkuu wa Sheria atekeleze kazi yake vilivyo."
}