GET /api/v0.1/hansard/entries/285248/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 285248,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/285248/?format=api",
    "text_counter": 755,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Namwamba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 108,
        "legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
        "slug": "ababu-namwamba"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, mabadiliko katika Idara ya Polisi na usalama kwa ujumla ni swala moja ambalo lilikuwa swala nyeti na sugu. Swala hili liliwapelekea Wakenya wengi kupigania mabadiliko ya kikatiba katika nchi hii. Ninaunga mkono Ripoti hii kwa sababu huu ni mwanzo wa safari ya kubadilisha sura ya Idara Ya Polisi. Ni safari ya kupiga msasa idara hii ili ipate sura mpya. Tuondoke kwenye zile siku ambazo askari walikuwa na tabia ya kuwanyanyasa wananchi bila ya sababu yeyote na kuingia katika mwamko mpya. Hapo zamani ukitoka kujivinjari na ukutane na askari, swali lilikuwa ni hili: “Wewe unatoka wapi?” Mengi ya maswali yao hayakustahili kuulizwa kwa sababu hawakuwa na heshima kwa mwananchi."
}