GET /api/v0.1/hansard/entries/285249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 285249,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/285249/?format=api",
"text_counter": 756,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Namwamba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 108,
"legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
"slug": "ababu-namwamba"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ninaiomba Bodi hii kuleta mabadiliko mwafaka katika idara hii. Kwa mfano, kumekuwa na tetesi kali ya kuwa usimamizi wa idara ya usalama huegemea upande mmoja wa taifa au baadhi ya maofisa wakuu wanatoka sehemu au kabila fulani. Tunataka kuona sura ya Kenya katika usimamizi wa idara ya polisi. Ninataka Bodi hii itilie maanani swala hili ili kuwe na usawa katika usimamizi wa idara hii. Hatutaki kusikia usemi kama ule wa Waziri wa Usalama, mhe. Profesa George Saitoti, kuwa hawezi kupata watu ambao wanaweza kusimamia idara ya polisi kutoka makabila fulani katika taifa hili. Nimeshangaa kusikia hatuwezi kupata watu ambao wanaweza kusimamia idara ya polisi kutoka kwa Mijikenda, Ndorobo na makabila mengine ya taifa hili."
}